• HABARI MPYA

    Tuesday, May 10, 2016

    HAJIB ATUA AFRIKA KUSINI KUJARIBU BAHATI

    MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Ibrahim Hajib yuko Johannesburg, Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio ya katika moja ya klabu tatu, zikiwemo Kaizer Chiefs ya nchini humo.
    Hajib aliondoka nchini jana asubuhi, ikiwa ni siku moja tangu atolewe kwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara timu yake, Simba ikilala 1-0 mbele ya Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Taifa, Jumapili.
    Ibrahim Hajib (kulia) wakati anaondoa jana

    Na kwa sababu kwa kadi Hajib asingeweza kucheza mechi mbili kati ya tatu za mwisho za Simba, akapna ni wakati mwafaka kutimiza mpango wake wa kwenda kujaribu bahati yake sehemu nyingine. 
    Hajib ameondoka na mdau mkubwa wa Simba SC, Juma Ndabila ambaye pia ni promota a bondia Francis Cheka.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba uongozi haufahamu lolote kuhusu safari ya Hajib.
    Aidha, Poppe amesema kwamba lakini hawana waiwasi kwa sababu mchezaji huyo ana Mkataba wa mwaka mmoja zaidi Simba. Kila la heri kwa Hajib.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HAJIB ATUA AFRIKA KUSINI KUJARIBU BAHATI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top