• HABARI MPYA

    Friday, May 20, 2016

    SERENGETI BOYS NA KOREA KUSINI KATIKA PICHA JANA INDIA

    Kiungo wa Tanzania, Shaaban Zuberi Ada (kushoto) akijivuta kupga krosi mbele ya beki wa Korea Kusini, Lee Soobin katika mchezo wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 16, maarufu kama AIFF Younth Cup jana Uwanja waTilak Maidan Goa India. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2 na Serengeti Boys kutinga Nusu Fainali ikiwa imebakiza mchezo mmoja dhidi ya Malaysia kesho
    Kiungo wa Korea Kusini, Park Jeongin akipiga kichwa mbele ya mchezaji wa Serengeti Boys, Issa Abdi Makamba
    Kiungo wa Tanzania, Asad Ally akimlamba chenga beki na Nahodha wa Korea, Kim Taehwan
    Kipa wa Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili (kulia) akishuhudia mpira ukitinga nyavuni baada ya Joung Sungiune (kushoto) kuifungia Korea bao la pili. Mwingine pichani ni Nahodha wa Serengeti Boys, Issa Abdi
    Kikosi cha Serengeti Boys katika mchezo wa jana
    Kikosi cha Korea Kusini katika mchezo wa jana 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS NA KOREA KUSINI KATIKA PICHA JANA INDIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top