• HABARI MPYA

    Friday, May 20, 2016

    MAPOKEZI YA YANGA LEO UWANJA WA NDEGE, NYOMI LA KUFA MTU!

    Mashabiki wa Yanga 'wakimgombania' kipa wa timu yao, Deo Munishi 'Dida' wakati timu ilipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam mchana wa leo kutoka Angola ambako iliwatoa wenyeji Sagrada Esparanca mjini Dundo juzi kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya kushinda 2-0 nyumbani na kufungwa 1-0 juzi ugenini, hivyo kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika

    Dida akiwaonyesha ishara ya upendo mashabiki wa Yanga baada ya kutoka nje ya JNIA
    Nahodha Nadir Haroub Cannavaro akitoka ndani ya JNIA kuelekea kwenye basi
    Kiungo kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima akitoka ndani ya JNIA kuelekea kwenye basi
    Mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma akitoka ndani ya JNIA kuelekea kwenye basi
    Beki Vincent Bossou kutoka Togo akitoka ndani ya JNIA kuelekea kwenye basi
    Mashabiki wa Yanga wakiliongoza basi la wachezaji wao kuelekea makao makuu ya klabu, Jangwani
    Mashabiki wa Yanga wakaifuaria kwa shangwe mbele ya basi la wachezaji wao likielekea Jangwani
    Kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko akielekea kwenye basi baada ya kutoka nje ya JNIA 
    Shabiki huyu alidandia kwenye kioo cha basi ili awapongeze wachezaji wa timu yake
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAPOKEZI YA YANGA LEO UWANJA WA NDEGE, NYOMI LA KUFA MTU! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top