• HABARI MPYA

  Tuesday, May 10, 2016

  PATI LA UBINGWA YANGA NI JUMAMOSI TAIFA BAADA YA MECHI NA NDANDA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji, Ndanda FC na Yanga uliokuwa ufanyike Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara sasa utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi.
  Hiyo inafuatia makubaliano ya timu hizo, Yanga na Ndanda FC ambayo yamebarikiwa na Bodi ya Ligi pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
  Yanga iliipigia magoti Ndanda FC kuomba mechi ichezwe Dar es Salaam kwa sababu wanataka kuwahi Angola Mei 17 kucheza na wenyeji Sagrada Esperanca katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kwenda hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

  Na Ndanda wamekubali kucheza mechi zote mbili za msimu na Yanga ugenini, kwa sababu hawana cha kupoteza wala kupata zaidi katika Ligi Kuu ilipofikia.  
  Katika mchezo huo, Yanga itakabidhiwa Kombe lake la ubingwa wa Ligi Kuu, iliyojihakikishia Jumapili baada ya Simba SC kufungwa bao 1-0 na Mwadui FC jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Matokeo hayo yanamaanisha hakuna timu yoyote ya Ligi Kuu yenye uwezo wa kufikisha pointi 68 ambazo wanazo Yanga hadi sasa – na bila ubishi timu ya Jangwani imetetea ubingwa.
  Simba SC ina pointi 58 baada ya kucheza mechi 27 na inaweza kufikisha pointi 67 ikishinda mechi zake zote tatu zilizobaki, wakati Azam FC inaweza kumaliza na pointi 66. 
  Yanga leo wanacheza na Mbeya City uwanja wa Sokoine mjini Mbeya katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PATI LA UBINGWA YANGA NI JUMAMOSI TAIFA BAADA YA MECHI NA NDANDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top