• HABARI MPYA

  Tuesday, May 10, 2016

  MCHEZAJI MWINGINE WA CAMEROON AZIMIA NA KUFARIKI DUNIA UWANJANI

  KIPA wa timu ya wanawake ya Cameroon amefariki dunia baada ya kuzimia kabla ya mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza, ndani ya saa 48 baada ya kifo cha Patrick Ekeng, Shirikisho la Soka la nchi hiyo limesema Jumatatu.
  Jeanine Christelle Djomnang (pichani kushoto), mwenye umri wa miaka 26, alianguka wakati wa mazoezi ya kuamsha misuli kabla ya mechi ya Femina Stars Ebolowa Jumapili, ingawa sababu za kifo chake bado hazijajulikana na inasubiriwa taarifa ya kitabibu.
  Kifo cha kipa huyo wa timu ya wanawake, kinafuatia kifo cha kiungo wa kimataifa wa Cameroon, Ekeng, aliyezimia wakati wa mechi ya Daraja la Kwanza Romania akiichezea timu yake, Dinamo Bucharest usiku wa Ijumaa.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alianguka uwanjani bila ya kuguswa na mchezaji yeyote dakika ya 70 katika mchezo dhidi ya Viitorul, dakika saba tu taangu aingine kutokea benchi.
  Alikimbizwa hospitali, lakini madaktari wakashindwa kuokoa maisha yake.
  Vifo vya Djomnang na Ekeng vimewakumbusha miaka 13 iliyopita wapenzi wa soka wa Cameroon wakati kiungo wa zamani wa kimataifa wa timu hiyo, Marc-Vivien Foe alipofariki dunia akiwa ana umri wa miaka 28 baada ya kuanguka na kupoteza fahamu mwaka 2003 kwenye Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Mabara la FIFA mjini Lyon, Ufaransa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHEZAJI MWINGINE WA CAMEROON AZIMIA NA KUFARIKI DUNIA UWANJANI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top