• HABARI MPYA

  Monday, May 09, 2016

  MALIMI BUSUNGU AMEMALIZA MSIMU YANGA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Yanga, Malimi Busungu amelazwa katika hospitali ya jeshi la Polisi barabara ya Kilwa, Dar es Salaam akipatiwa matibau.
  Busungu alishindwa kuendelea na mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika dhidi ya Sagrada Esparanca ya Angola juzi, baada ya kugongana na kipa Yuri JKose Tavazes.
  Malimi Busungu akiwa katika hospitali ya Polisi, barabara ya Kilwa

  Busungu aliumia mbavu na kutolewa kwa machela dakika ya 53 nafasi yake ikichukuliwa na Godfrey Mwashiuya, kabla ya kukimbizwa moja kwa moja hospitali.
  Baada ya uchunguzi wa awali, imeonekana Busungu amepata maumivu makubwa na hataweza kucheza kwa mwezi mmoja.
  Na bado Busungu anafanyiwa uchunguzi zaidi ili kujua ameumia kiasi gani na imeelezwa atakuwa katika hospitali hiyo ya jeshi la Polisi kwa wiki yote hii. 
  Katika mchezo wa juzi, Yanga ilishinda 2-0, mabao ya Simon Happygod Msuva na Matheo Antony Simon kipindi cha pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALIMI BUSUNGU AMEMALIZA MSIMU YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top