• HABARI MPYA

  Wednesday, April 20, 2016

  SIMBA YAMSIMAMISHA HASSAN KESSY, YAMPUNGIA MKONO WA KWAHERI BANDA

  Hassan Kessy amesimamishwa Simba
  Na Saada Mohammed , DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imemsimamsha mechi tano beki wake, Hassan Ramadhani Kessy kwa kumchezea rafu isiyo ya kimchezo mshambuliaji wa Toto Africans, Edward Christopher.
  Simba ilifungwa 1-0 na Toto Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Kessy akatolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 47 kwa kumchezea rafu Edward, nyota wa zamani wa timu hiyo Msimbazi.
  Pamoja na kumfungia, kocha Jackson Mayanja amewaomba radhi mashabiki wa Simba kwa matokeo hayo na kusema wanarakebisha makosa yao washinde mechi zijazo.
  Mganda huyo ameshauri kikosi kisibomolewe hata kama Simba itakosa taji msimu huu, ili kiboreshwe na msimu ujao kirejee na nguvu mpya.
  Kuhusu kiungo Abdi Banda, kocha huyo amesema mchezaji huyo hajafukuzwa bali amejiondoa mwenyewe kwenye timu baada ya kususa.
  Baada ya kupoteza mchezo na Toto kwa bao pekee la Waziri Junior dakika ya 20, Simba inabaki na pointi zake 57 baada ya kucheza mechi 25, ikiendelea kuwa nafasi ya pili, mbele ya Azam FC yenye pointi 55 za mechi 24, wakati Yanga wenye pointi 59 za mechi 24 wapo juu yao. 
  Wakati huo huo: Simba SC inatarajiwa kuingia kambini visiwani Zanzibar Ijumaa kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC Mei 1, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAMSIMAMISHA HASSAN KESSY, YAMPUNGIA MKONO WA KWAHERI BANDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top