• HABARI MPYA

  Wednesday, April 20, 2016

  MAN UNITED WATWAA TENA UBINGWA WA LIGI KUU YA VIJANA ENGLAND

  TIMU ya Manchester United imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa vijana chini ya umri wa miaka 21 kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kuifunga mabao 3-2 Tottenham jana Uwanja wa White Hart Lane.
  Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Andreas Pereira, Donald Love na Guillermo Varela na hilo linakuwa taji la tatu kwa kikosi cha Warren Joyce ndani ya miaka ya minne.
  Ushindi huo unawafanya United wafikishe pointi 45 katika msimamo wa Ligi Kuu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 England baada ya kucheza mechi 20, wakifuatiwa na Sunderland yenye pointi 43 za mechi 22.
  Sunderland imemaliza mechi zake,wakati Man United ina viporo viwili dhidi ya Southampton na Chelsea.
  Wachezaji wa U-21 ya Manchester United wakisherehekea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England kabla ya kumaliza Ligi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED WATWAA TENA UBINGWA WA LIGI KUU YA VIJANA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top