• HABARI MPYA

  Wednesday, April 20, 2016

  KENYA YAFUTWA MICHUANO YA VIJANA AFRIKA KWA KUTUMIA 'VIBABU'

  Erick Ouma Otieno anachezea Gor Mahia Ligi Kuu Kenya 
  KAMATI ya Mashindano ya vijana ya umri wa miaka 20 ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imeiondoa Kenya kwenye mechi za kufuzu fainali za U-20 mwaka 2017 Zambia.
  Hiyo inafuatia Kenya kutumia wachezaji waliozidi umri katika mchezo wa Raundi ya Kwanza dhidi ya Sudan Aprili 3 mwaka huu Uwanja wa El Merreikh, uliomalizika kwa sare ya 1-1.
  Wachezaji hao ni Erick Ouma Otieno aliyezaliwa Septemba 27, mwaka 1996,Nicholas Kipkirui, aliyezaliwa Mei 31, 1996,
  Boniface Muchiri, aliyezaliwa Agosti 23, 1996, Eugene Moses Mukangula, aliyezaliwa Juni 22, mwaka 1996 na Theodore Kibet Kilele, aliyezaliwa Septemba 25, mwaka 1996.
  Taarifa ya CAF kwa BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE imesema kwamba mashindano hayo ni kwa ajili ya vijana waliozaliwa kuanzia Januari 1, mwaka 1997.
  Taarifa hiyo ya Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani imesema Shirikisho la Soka Kenya (FKF) linaweza kukata rufaa ndani ya siku tatu..
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KENYA YAFUTWA MICHUANO YA VIJANA AFRIKA KWA KUTUMIA 'VIBABU' Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top