• HABARI MPYA

  Thursday, April 14, 2016

  SIMBA ‘WAITOLEA MACHO’ YANGA NA MTIBWA JUMAMOSI TAIFA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  YANGA SC itarudi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi kumenyana na Mtibwa Sugar katika kiporo chake cha mwisho cha Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mchezo ambao mahasimu wao, Simba watakuwa wanautazama kwa jicho la tatu.
  Simba inaiombea mabaya Yanga ipoteze mchezo au hata ipate sare ili iendelee kuwa katika nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
  Na Yanga kwa kulijua hilo, wanajiandaa kikamilifu kuhakikisha wanavuka na mtihani huo pia, ili waweke hai matumaini ya kutetea ubingwa wao.

  Simba SC yenye pointi 57 za mechi 24, ndiyo inaongoza Ligi Kuu ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 56 baada ya kucheza mechi 23, wakati Azam FC yenye pointi 55 za mechi 24 ni ya tatu.
  Bado mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ni za timu tatu zilizo juu, yaani Simba, Yanga na Azam na kulingana na mwenendo wa ligi hiyo ulivyo kwa sasa ni pigo kubwa kwa timu kupoteza pointi.  
  Iwapo Yanga wataifunga Mtibwa Jumamosi waterejea kileleni kwa mara ya kwanza mwezi huu, ingawa wanaweza wakadumu kwa saa kadhaa tu, kwani Simba wakishinda dhidi ya Toto Africans Jumapili Dar es Salaam watapanda tena juu.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu Jumamosi ni kati ya Coastal Union na JKT Ruvu Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ndanda FC na Kagera Sugar Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA ‘WAITOLEA MACHO’ YANGA NA MTIBWA JUMAMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top