• HABARI MPYA

    Thursday, April 14, 2016

    JULIO ASHAURI AZAM, SIMBA YANGA ZITENGEWE LIGI YAO

    Na Saada Mohammed, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Mwadui FC, Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’ ameishauri TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) kuanzisha ligi ya timu tatu, Azam, Simba na Yanga zicheze peke yao.
    Ushauri wa Julio umetokana na kukerwa na kile anachoamini timu hizo tatu za Dar es Salaam zinapendelewa katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinapoocheza na timu nyingine.
    Na ushauri huo aliutoa muda mfupi baada ya mchezo wa Ligi Kuu jana dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    “Marefa wamewapendelea waziwazi wapinzani wetu hadi wameshinda, kwa kweli hii siyo sawa ndiyo maana mimi nasema bora tu TFF ianzishe ligi ya timu tatu tujue moja,”amesema.
    Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo (kulia) jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

    Yanga jana imeendeleza wimbi la ushindi katika mashindano ya nyumbani baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Shukrani kwake, kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima aliyefunga bao la ushindi mwishoni kipindi cha pili, baada ya kubanwa kiasi cha kutosha na Mwadui.
    Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 56 baada ya kucheza mechi 23, ikiendelea kukaa nafasi ya pili nyuma ya Simba SC yenye pointi 57 za mechi 24. 
    Yanga walitangulia kupata bao kupitia kwa Simon Msuva aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Issoufou Boubacar, kabla ya Mwadui kusawazisha dakika ya 13 kupitia kwa mshambuliaji Kelvin Sabati aliyeukuta mpira uliopanguliwa na kipa Deo Munishi ‘Dida’ baada ya shuti lake mwenyewe.
    Bao hilo lilitokana na makosa ya kiungo Mzimbabwe wa Yanga, Thabani Kamusoko aliyepiga mpira ukanaswa na kiungo wa Mwadui, Razack Khalfan nje kidogo ya boksi akampasia Sabati aliyefunga.
    Refa Selemani Kinugani alimtoa kwa kadi nyekundu, Iddi Mobby dakika ya 70 kwa kumchezea rafu kiungo wa Yanga, Kamusoko kabla ya Yanga kupata bao la pili dakika ya 86, baada ya Niyonzima kupiga shuti kali kufuatia pasi ya kichwa ya mshambuliaji Donald Ngoma.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JULIO ASHAURI AZAM, SIMBA YANGA ZITENGEWE LIGI YAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top