• HABARI MPYA

  Wednesday, April 06, 2016

  SIMBA SASA YAAMUA KUIONGEZEA KASI YANGA MBIO ZA UBINGWA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imesema kwamba itaendelea kucheza mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, licha ya wapinzani wao, Yanga kuendelea kuwekewa vipro.
  Awali, Simba ilitangaza kutocheza mechi zake hadi Yanga na Azam wakamilishe mechi zao za viporo, lakini leo wamekuja kauli mbadala wakidai eti wameshitukia mtego wa kushushwa daraja.
  Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Simba, Hajji Sunday Manara amesema kutokana na kugundua hilo wao kama Simba wanaitupia
  lawama bodi ya Ligi ambayo imekuwa ikibadili ratiba mara kwa mara.
  Simba SC itaendelea kucheza mechi zake za Ligi Kuu licha ya Yanga kuongezewa viporo

  “Haiwezekani Yanga ishindwe kucheza mechi ya jana (na Mtibwa Sugar), halafu ikubali kucheza Aprili 16, wakati tarehe hizo wanatakiwa wawe Misri kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly,"amesema Manara.
  Amesema hizo ni dalili za bodi ya Ligi na TFF kuitengenezea mazingira Yanga ya kutetea ubingwa kiulaini.
  Manara pia amesema wana wasiwasi mchezo wa Yanga na Mtibwa uliosogezwa kutoka jana hadi Aprili 16 utaahirishwa tena kwa sababu wapinzani wao hao katika mbio za ubingwa watakuwa wanasafiri kwenda Misri katika mechi ya marudiano na Al Ahly.
  Simba SC ndiyo inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 57 za mechi 24, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 53 za mechi 22, wakati Azam FC yenye pointi 52 za mechi 23 ni ni ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SASA YAAMUA KUIONGEZEA KASI YANGA MBIO ZA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top