• HABARI MPYA

  Wednesday, April 20, 2016

  MAZEMBE YAVULIWA UBINGWA WA AFRIKA NA WAARABU

  TIMU ya TP Mazembe imevuliwa ubingwa wa Afrika baada ya kutolewa Wydad Casablanca katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia sare ya 1-1 jioni ya leo Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, DRC.
  Matokeo hayo yanafanya Mazembe itolewe kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya wiki iliyopitwa kufungwa 2-0 Morocco.
  Mazembe ilitangulia kwa bao la Coulibaly aliyemalizia pasi ya Solomon Asante dakika ya 28, kabla ya Reda Hajhouj kuwasawazishia wageni dakika ya 90 na ushei.
  Mechi nyingine ya leo, ASEC Mimosa imefuzu hatua ya makundi licha ya kufungwa 2-1 na Ahly Tripoli Uwanja wa Chedly-Zouiten mjini Tunis.

  ASEC inafuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kushinda 2-0 mjini Abidjan.
  Zote, ASEC na Wydad zinaungana na Zamalek ya Misri, ES Setif ya Algeria na Zesco United ambazo zilifuzu baada ya mechi za jana.
  Zamalek inafuzu baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na Mouloudia Bejaia ya Algeria katuika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora na kusonga mbele kwa ushindi wa 3-1 baada ya awali kushinda 2-0 nyumbani.
  Zesco United imeshinda 2-1 jana dhidi ya Stade Malien ya Mali mjini Ndola na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 5-2 baada ya kushinda 3-1 mjini Bamako.
  ES Setif ya Algeria wametoa sare ya 0-0 na El Merreikh na kusonga mbele kwa mabao ya ugenini baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Sudan.
  Mechi nyingine za leo ni kati ya; Al Ahly ya Misri na Yanga SC ya Tanzania, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na AS Vita Club ya DRC na ES Sahel ya Tunisia dhidi ya Enyimba Nigeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAZEMBE YAVULIWA UBINGWA WA AFRIKA NA WAARABU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top