• HABARI MPYA

  Wednesday, April 20, 2016

  MALINZI AWAPOZA MACHUNGU AZAM, AWAOMBEA DUA NJEMA YANGA SC LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewafariji Azam FC baada ya kutolewa katika michuano ya Afrika.
  Azam FC jana imeaga michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika baada ya kufungwa mabao 3-0 na wenyeji Esperance katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Uwanja wa Olimpiki Novemba 7 mjini Rades, Tunis, Tunisia.
  Matokeo hayo yanafanya Azam FC inayomilikiwa na bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake itolewe kwa jumla ya mabao 4-2, baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam.

  Na Malinzi amewataka Azam FC kujipanga upya ili wakipata nafasi ya kucheza tena michuano ya Afrika mwakani wafanye vizuri.
  “Kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi, Azam warudi wajipange inshaallah, wakipata fursa nyingine watafanya vizuri zaidi,”amesema Malinzi.
  Pamoja na hayo, Malinzi amewatakia kila la kheri Yanga SC ambao leo wanamenyana na wenyeji Al Ahly Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Yanga inatakiwa kushinda ugenini baada ya wiki iliyopita kulazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam.
  Wakati huo huyo: Rais Malinzi amesema TFF ipo katika mchakato wa kukusanya maoni kwa wadau wake juu ya mfumo wa uendeshwaji wa Ligi Kuu ya wanawake nchini.
  “Msimu wa 2016/17 TFF itaanzisha ligi kuu ya klabu za wanawake Tanzania (TWPL). Ligi hii itaanza na klabu 10 tu, hii itakuwa chachu kubwa ya kupata Tanzanite na Twiga Stars bora,”.
  “Kama mnavyofahamu ni maeneo machache Tanzania klabu za wanawake zinacheza ligi, tunakusanya ushauri wa namna ya  kupata timu 10 za kwanza kwa ajili ya ligi hiyo,”amesema Malinzi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALINZI AWAPOZA MACHUNGU AZAM, AWAOMBEA DUA NJEMA YANGA SC LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top