• HABARI MPYA

  Tuesday, April 05, 2016

  AL AHLY KUTUA NA WAPIGANAJI 21 KESHO

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha mabingwa wa zamani wa Afrika, Al Ahly ya Misri kinatarajiwa kuwasili kesho Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo dhidi ya Yanga Jumamosi.
  Timu hiyo ya kocha Mholanzi, Maarten Cornelis Jol maarufu kama Martin Jol, itawasili na ndege maalum ya kukodi tayari kwa mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Ahly inatarajiwa kufikia katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam na itakuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana Club hadi Ijumaa itakapohamia Uwanja wa Taifa.
  Na kikosi kinachotarajiwa kutua kesho ni makipa; Ahmed Abdul Monem, Mosaad Awad, Sherif Ekramy.
  Kikosi cha Al Ahly kilichomenyana na Yanga mwaka juzi katika Ligi ya Mabingwa 

  Mabeki; Ahmed Fathy, Bassem Ali, Mohamed Hany, Rami Rabia, Saad Samir, Ahmed Hagazy na Sabri Rahil.
  Viungo; Amir El-Sulaya, Ahmed El El- Sheikh, Walid Soliman, Abdalla El Said, Hossam Ghaly, Hossam Ashour, Ramadan Sobhi na Momen Zakaria.
  Washambuliaji; Malick Evouna, Emad Moteab na Amr Gamal.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL AHLY KUTUA NA WAPIGANAJI 21 KESHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top