• HABARI MPYA

    Thursday, March 10, 2016

    YANGA WAFIKIA BONGE LA HOTELI KIGALI, KUJIFUA KWENYE NYASI BANDIA LEO

    KIKOSI CHA YANGA KILICHOPO KIGALI;
    Makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’.
    Mabeki; Juma Abdul, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Kevin Yondani, Pato Ngonyani.
    Viungo; Thabani Kamusoko, Said Juma, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke na Issofou Boubacar.
    Washambuliaji; Paul Nonga, Donald Ngoma, Matheo Anthony, Amissi Tambwe na Paul Nonga.
    BENCHI LA UFUNDI;
    Kocha Mkuu; Hans van der Pluijm (Uholanzi)
    Kocha Msaidizi; Juma Mwambusi
    Kocha wa makipa; Juma Pondamali
    Daktari; Edward Bavu
    Mchua Misuli; Jacob Onyango
    Mtunza Vifaa; Mohammed Mpogolo
    Meneja; Hafidh Saleh
    WACHEZAJI WALIOBAKI DAR;
    Benedicto Tinocco, Nadir Haroub 'Cannavaro', Malimi Nusungu na Godfrey Mwashiuya.
    Hoteli ya kifahari ya Mirror mjini Kigali, Rwanda ambayo wamefikia Yanga

    Na Prince Akbar, KIGALI
    KIKOSI cha Yanga kimewasili salama mjini Kigali, Rwanda tayari kwa mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, APR Jumamosi, Uwanja wa Amahoro mjini Kigali Rwanda.
    Yanga imefikia katika hoteli ya kifahari ya Mirror mjini Kigali, wakati jioni ya leo itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa nyasi wa bandia wa Shirikisho ya Soka la Rwanda (FERWAFA).
    Kesho Yanga watafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Amahoro ambao ndio utatumika kwa mchezo huo jioni ya Jumamosi. 
    Yanga imetua Rwanda karibu na kikosi chake kizima, ili wachezaji wote waendelee na programu za mazoezi kwa ajili ya mechi zijazo, zikiwemo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na marudiano dhidi ya APR wiki ijayo.   
    Yanga SC itashuka Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda Jumamosi ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 3-0 mjini humo walipokutana mara ya kwanza na ya mwisho kwenye michuano mwaka 1996.
    Wachezaji wa Yanga wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ndege ya Rwanda Air kabla ya safari yao Uwanja wa Ndege wa KImataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam
    Wachezaji wa Yanga wakiwa kwenye ndege ya Rwanda Air kwa safari ya Kigali leo

    APR iliitoa Yanga katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa mwaka 1996 jumla ya mabao 3-1, ikishinda 3-0 Kigali kabla ya kuja kufungwa 1-0 Dar es Salaam.
    Miaka 20 baadaye, timu hizo zinakutana tena katika hatua ile ile – na michuano ile ile, tena kwa namna ile ile, Yanga wakianzia ugenini.
    Kocha Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm amesema kwamba wanakwenda kwenye mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya APR, lakini watapambana wasipoteze.
    Pluijm amesema kwamba mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, utakuwa mgumu kwa sababu APR ni timu nzuri.
    “APR ni timu nzuri na watakuwa wamejiandaa vizuri, lakini sisi tuko vizuri, tutakwenda kupambana tusipoteze mchezo, ili tumalizie vizuri mchezo wa nyumbani,”amesema.
    Kwa upande wake, kocha mpya wa APR, Nizar Khanfir amesema kwamba amewaona Yanga katika video na anataka kuwafunga Jumamosi.
    “Lengo letu ni kushinda huo mchezo"amesema na kuongeza; "Nimeona baadhi ya video zao na tutaendelea kuwachambua katika siku chache zijazo kuelekea kwenye mechi,”.
    Mechi hiyo inatarajiwa kuchezeshwa na marefa wa Malawi Jumamosi Uwanja wa Amahoro, Kigali Rwanda.
    Duncan Lengani anatarajiwa kupuliza filimbi, wakati washika vibendera watakuwa Clemence Kanduku na Jonizio Luwizi.
    Mchezo wa marudiano wiki moja baadaye Dar es Salaam, utachezeshwa na marefa wa Shelisheli; katikati Bernard Camille na pemebeni watakuwapo Eldrick Adelaide na Gerard Pool. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAFIKIA BONGE LA HOTELI KIGALI, KUJIFUA KWENYE NYASI BANDIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top