• HABARI MPYA

  Friday, March 11, 2016

  YANGA NA APR AMAHORO ‘LIVE BILA CHENGA’ AZAM TV KESHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM TV imeingia Mkataba na APR kuonyesha mechi ya kwanza ya Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wageni wao, Yanga kesho Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda.
  Na Azam TV ambayo inaongoza kwa sasa kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa huduma hiyo itaonyesha moja kwa moja mchezo huo kesho kuanzia Saa 10:30 kwa saa za Afrika Mashariki.
  Wapiga picha, mafundi mitambo, wachambuzi na watangazaji wa Azam TV tayari wako mjini Kigali, Rwanda na leo wamehudhuria mazoezi ya Yanga Uwanja wa Amahoro kwa matayarisho ya awali.
  Mashabiki wa Yanga watashuhudia mchezo wa timu yao na APR kupitia Azam TV kesho

  Wapenzi wa Yanga nchini wameipokea kwa furaha kubwa hatua ya Azam TV kuamua kurusha mechi za timu yao ikicheza nje ya nchi.
  “Kwa kweli mimi ninaipongeza sana Azam TV kwa hatua hii, inatusaidia mno wapenzi kuweza kuzifuatilia timu zetu zikicheza nje, tunaomba waendelee na moyo huo,”amesema Ibrahim Ramadhani wa Temeke.
  Naye Fatuma Issa maarufu ‘Fatuma Yanga’ wa Magomeni amesema kwamba kesho kuanzia saa 8:00 mchana atakuwa mbele ya Televisheni yake kufuatilia mchezo huo na anaitakia kila la heri timu yake, Yanga iifunge APR.
  Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Muingereza Rhys Torrington amesema kwamba utamaduni huo utaendelea kwa mechi zote za Yanga na hata timu nyingine zinazoliwakilisha taifa.  
  “Hatujaanza leo, tumeanza miaka miwili iliyopita. Na tutaendelea. Hii si kwa Yanga tu, bali kwa timu zote zinazowakilisha nchi, kikubwa ni kupata haki kwa wenyeji,”amesema Torrington.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA APR AMAHORO ‘LIVE BILA CHENGA’ AZAM TV KESHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top