• HABARI MPYA

  Thursday, March 03, 2016

  REDONDO: HISTORIA ITAIBEBA MBEYA CITY DHIDI YA SIMBA JUMAPILI TAIFA

  Redondo amesema historia itaibeba Mbeya City mbele
  ya Simba Jumapili Uwanja wa Taifa
  Na Doreen Favel, MBEYA
  KIUNGO wa Mbeya City, Ramadhani Chombo 'Redondo' amesema historia itawabeba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Redondo amesema Mbeya City ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo kwa sababu imekuwa na historia nzuri kila inapokutana na Simba kwenye uwanja wa Taifa.

  “City imeshinda mara kadhaa mbele ya Simba, hili ni jambo zuri kisaikolojia, kwa sababu linaleta kujiamini, imani yangu kubwa dakika 90 za Jumapili zitakuwa nzuri upande wetum” alisema.
  Hata hivyo, kiungo huyo wa zamani wa Ashanti, Simba na Azam FC, amesema kwamba mchezo huo utakuwa mgumu kwa sababu timu zote zitakutana zikitoka kupoteza mechi zake zilizopita za Ligi Kuu.
  “Ni wazi utakuwa mgumu, hii ni kwa sababu kila timu inahitaji matokeo mazuri baada ya kupoteza mchezo uliopita, Simba na timu nzuri na wako kwenye nafasi nzuri pia, lakini wasitegeme kupata ushindi kwa sababu sisi tunauhitaji zaidi yao,” alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REDONDO: HISTORIA ITAIBEBA MBEYA CITY DHIDI YA SIMBA JUMAPILI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top