• HABARI MPYA

  Friday, March 04, 2016

  MESSI AGONGA HAT TRICK BARCELONA IKIMPA MTU 5-1 LA LIGA

  BARCELONA imezidi kukimbia kivuli chake katika Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga baada ya ushindi wa mabao 5-1 usiku huu dhidi ya wenyeji Rayo Vallecano Uwanja wa Rayo Vallecano mjini Madrid.
  Mwanasoka bora kabisa kuwahi kutokea duniani, Lionel Messi amefunga mabao matatu peke yake usiku huu katika dakika za 23, 53 na 72, huku mabao mengine ya Barca yakifungwa na Ivan Rakitic dakika ya 22 na Arda Turan dakika ya 86.

  Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia mabao matatu peke yake barceloma ikishinda 5-1 dhidi ya Rayo Vallecano katika La Liga PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Bao pekee Rayo Vallecano limefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Angola, Manucho Goncalves dakika ya 57 na sasa Barca inafikisha pointi 66 baada ya kucheza mechi 26 na kuendelea kujinafasi kileleni mwa La Liga, ikifuatiwa na Atletico Madrid yenye pointi 61 za mechi 27 na Real Madrid yenye pointi 57 za mechi 27 pia.
  Rayo Vallecano inabaki na pointi zake 26 za mechi 26 na kuendelea kushika nafasi ya 16 katika ligi ya timu za 20. 
  Katika mchezo huo, Rayo iliwapoteza wachezaji wake wawili waliotolewa kwa kadi nyekundu, Diego Llorente aliyemchezea vibaya Rakitic dakika ya na Manuel Iturra aliyemuangusha Luis Suarez kwenye boksi. Lakini Suarez alikosa penalti iliyotolewa baada ya kuangushwa kwake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI AGONGA HAT TRICK BARCELONA IKIMPA MTU 5-1 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top