• HABARI MPYA

    Sunday, March 13, 2016

    MKUU WA MKOA TANGA AITAKA TFF KUFANYIA KAZI SOKA YA WANAWAKE

    MKUTANO Mkuu wa Shirikisho la Soka (TFF) umeahirisha mpango wa marekebisho ya Katiba hadi katika Mkutano Mkuu ujao, unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huuu.
    Mkutano huo Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera mini Tanga na kuhudhuriwa na mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahizab, baada ya majadiliano ya kina ulikubali kuahirisha ajenda ya marekebisho ya Katiba.
    Katika hotuba yake kwa wajumbe wa mkutano huo, Mahiza aliushukuru uongozi wa TFF nchini kwa kuweza kuandaa mkutano mkuu mzuri na wa kisasa ambao pia ulifanyikia katika mkoa wake wa Tanga.
    Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza (kushoto) na Rais wa TFF, Jamal Malinzi wakati wa kuweka jiwe la msingi wa Tanga Academy

    Akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu, Mahiza alisema, TFF ina changamoto ambazo inapaswa kuzifanyia kazi kwa na hasa katika kuendeleza soka la wanawake nchini ambalo bado mwamko wake uko chini sana.
    Mahiza alisema, Mpira wa miguu kwa sasa ni ajira nzuri ambayo inasaidia kujikwamua kiuchumi kwa wachezaji pamoja na familia zao, nayaomba makamouni yajitokeze kuwekeza katika mpira wa miguu na hasa katika soka la wanawake.
    “Mahitaji ya wanawake katika kushiriki/kucheza mpira wa miguu ni makubwa zaidi, tofauti na wanaume hivyo kuangalia jinsi gani wadhamini wanapatikana ili kuweza kuwasaidia wanawake” alisema Mahiza.
    Mkutano ulijadili Ajenda za kawaida ambazo ni Kufungua Mkutano ni Uhakiki wa Wajumbe, Kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita, Yatokanayo na Mkutano uliopita, Hotuba ya Rais, Taarifa kutoka kwa Wanachama, Kuthibitisha ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Utendaji.
    Zingine ni Kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013, Kuthibitisha ripoti ya Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu, Kupitisha bajeti ya 2015, Marekebisho ya Katiba, Mengineyo na Kufunga Mkutano.
    Wakati huo huo Leo Jumapili asubuhi Mkuu wa Mkoa Tanga, Mwantumu Mahiza ameweka jiwe la msingi katika eneo la kituo cha michezo cha kukuzia vipaji lilipo eneo la Mikanjuni jijini Tanga.
    Akiongea wakati wa uzinduzi wa uwekaji jiwe la msingi, Mahiza alisema wamejisikia faraja mkoa wa Tanga kupata nafasi hiyo kuwa mkoa wa kwanza kupata kituo cha kukuzia vipaji nchini.
    Mahiza alisema uongozi wa Serikali mkoa wa Tanga utashirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tanga (TRFA)/TFF katika kusaidia usimamizi wa uendeshaji wa kituo hicho.
    Mahiza ameishukuru TFF kwa kuamua kuwekeza katika ujezi wa kituo hicho, ambacho baaade kitatoa nafasi kwa vijana kupata ajira kupitia mpira na shughuli nyingine za maendeleo ya kiuchumi ikiwemo utalii na watu kupata ajira katika kituo hicho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKUU WA MKOA TANGA AITAKA TFF KUFANYIA KAZI SOKA YA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top