• HABARI MPYA

    Monday, March 23, 2026

    MANCHESTER CITY YAICHAPA ARSENAL 2-0 NA KUTWAA CAFRABAO CUP


    TIMU ya Manchester City FC jana ilifanikiwa kutwaa Kombe la Ligi England baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Fainali Uwanja wa Wembley Jijini London.
    Mabao yaliyoipa Manchester City taji la ya Carabao Cup yalifungwa na beki chipukizi wa kushoto wa umri wa miaka 21 ambaye pia hucheza nafasi za kiungo, Nico O'Reilly yote mawili dakika ya 60 na 64.
    Hilo linakuwa taji la tisa la Carabao kwa Manchester City baada ya awali kulibeba katika misimu ya 1970, 1976, 2014, 2016, 2018, 2019, 2020 na 2021.
    Mara ya mwisho Arsenal kutwaa taji iliuwa ni Agosti mwaka 2020 walipobeba Kombe la FA Cup chini ya kocha wa sasa, Mikel Arteta kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Chelsea kwenye Fainali hapo hapo Uwanja wa Wembley.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAICHAPA ARSENAL 2-0 NA KUTWAA CAFRABAO CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top