TIMU ya Pyramids FC imevuliwa ubingwa wa Afrika baada ya kuchapwa mabao 2-1 na AS FAR Rabat ya Morocco katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika usiku wa Jumamos Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 Jijini Cairo nchini Misri.
Mabao ya AS FAR Rabat yamefungwa na mshambuliaji Mmorocco, Reda Slim anayecheza kwa mkopo kutoka Aal Ahly ya Misri dakika ya tisa na kiungo Mohamed Rabie Hrimat dakika ya 54, wakati bao pekee la Pyramids limefungwa na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 62.
Kwa matokeo hayo, AS Rabat inakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-3 kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Machi 14 Uwanja wa Olimpiki Jijini Rabat nchini Miorocco.
Siku hiyo, mabao yote yalifungwa na mawinga, Ahmed Hammoudan akianza kuifungia AS FAR Rabat dakika ya nane, kabla ya Mahmoud Zalaka kuisawazishia Pyramids dakika ya 52.

.png)
0 comments:
Post a Comment