• HABARI MPYA

  Tuesday, March 15, 2016

  MISRI YATAMBA KUWAFUNGA NIGERIA KWAO

  KOCHA Msaidizi wa Misri, Mahmoud Fayez (pichani kulia) ameionya Super Eagles kwamba timu yake inakwenda Nigeria kuchukua pointi zote tatu.
  Mafarao wanaongoza Kundi G katika mbio za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 wakiwa na pointi sita na ushindi dhidi ya Nigeria utawafanya wafikishe wafikishe pointi tisa na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kuelekea mechi mbili za mwisho.
  Wachezaji watano wa kigeni watajiunga na kikosi cha Misri kwa kambi ambayo itaanza Machi 20 kabla ya kwenda Nigeria siku mbili kabla ya mechi.
  Fayez, ambaye ni miongoni mwa watu 11 wa benchi la Ufundi atakayeongozana na timu Nigeria, amesema Mafarao watakwenda Nigeria kwa lengo la kuchukua pointi tatu.
  "Tunafahamu kila kitu kuhusu Nigeria, tumekuwa tukiwasoma. Ni timu nzuri sana, lakini tuna mipango yetu sehemu ya kuwafungia”amesema.
  Nigeria watakuwa wenyeji wa Misri katika mchezo wa kwanza kati ya miwili mjini Kaduna Machi 25 Saa 10.00 jioni, mchezo ambao utaonyeshwa moja kwa moja na Supersport.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MISRI YATAMBA KUWAFUNGA NIGERIA KWAO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top