• HABARI MPYA

    Thursday, March 03, 2016

    MAN UNITED, LIVERPOOL ZOTE ZASHINDA..ARSENAL YALALA 2-1 ENGLAND

    Mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino akimrukia migongoni mshambuliaji wa Liverpoool, Divock Origi wakati wakimpongeza James Milner baada ya kufunga  PICHA ZIDI GOANGA HAPA


    TIMU ya Liverpool imeichapa mabao 3-0 Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Anfiled.
    Ushindi huo ni sawa na kisasi cha kufungwa kwa penalti 3-1 katika fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup Februari 28, Uwanja wa Wembley baada ya sare ya 1-1.
    Katika mchezo wa leo, mabao ya Liverpool yamefungwa na Adam Lallana dakika ya 34, James Milner dakika ya 41 na Roberto Firmino dakika ya 57.

    Nyota wa Manchester United, Juan Mata akidjangilia baada ya kuifungi timu yake pekee katika ushindi wa 1-0 victory over Watford PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya England usiku huu, Manchester United imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga 1-0 Watford, bao pekee la Juan Mata dakika ya 83 Uwanja wa Old Trafford.
    Arsenal imefungwa 2-1 nyumbani na Swansea City Uwanja wa Emirates katika mchezo mwigine wa ligi hiyo. Mabao ya Swansea yamefungwa na Wayne Routledge dakika ya 32 na Ashley Williams dakika ya 74, wakati la Gunners limefungwa na Joel Campbell dakika ya 15.

    Nahodha wa Swansea City akimtungua kipa wa Arsenal, Petr Cech katika mchezo wa Ligi ya England baada ya krosi ya Gylfi Sigurdsson Uwanja wa Emirates PICHA ZAIDI GONHA HAPA


    Stoke City imeilaza 1-0 Newcastle United, bao pekee la Xherdan Shaqiri dakika y 80 Uwanja wa Britannia.
    West Ham United imeilaza 1-0 Tottenham Hotspur, bao pekee la Michail Antonio dakika ya saba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED, LIVERPOOL ZOTE ZASHINDA..ARSENAL YALALA 2-1 ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top