• HABARI MPYA

    Wednesday, March 02, 2016

    MWAMBUSI: AZAM WAGUMU, LAKINI 'TUTAWANYOROSHA' TU

    Na Renatha Msungu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Msaidizi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Bara, timu ya soka ya Yanga, Juma Mwambusi, amesema pamoja na ugumu wa mchezo wao na Azam FC, kikosi chao kinahitaji kupata ushindi katika mechi hiyo, ili waweze kuendelea kukaa kileleni mwa Ligi Kuu ya bara inayoendelea katika viwanja tofauti hapa nchini.
    Yanga ambayo imeweka kambi kisiwani Pemba, kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo, na mechi nyingi za Ligi Kuu na Klabu bingwa Afrika, inatarajia kushuka dimbani Jumamosi kucheza na Azam FC, katika mchezo uliopangwa kufanyika kwenye uwanja wa taifa uliopo jijini Dar es Salaam.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE, Mwambusi amesema timu yao iko vizuri, inaendelea na mazoezi chini yake na Kocha Mkuu, Hans van der Pluijim, ili kuhakikisha wanashinda katika mechi hiyo ambayo ni muhimu kwao kupata pointi tatu.
    Kocha Mwambusi (kulia) akiwa na kipa wake, Ally Mustafa 'Barthez'

    Alisema kikosi chao kimewasili salama visiwani Pemba, kikiwa na wachezaji wote, kuendelea na maandalizi ya pambano hilo ambalo mashabiki walichukulia kama fainali kutokana kwamba timu zote zinapointi sawa na zinahitaji ushindi ili ziweze kukaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Bara.
    Mwambusi alisema, pamoja na ugumu wa mechi hiyo, Yanga imejianda vya kutosha, ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo, ambao unasubiriwa na mashabiki wengi wa soka, kitendo ambacho watakuwa wamejiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao.
    Akizungumzia kuhusiana na wachezaji majeruhi kwenye Kikosi hicho, alisema, wanaendelea vizuri na mazoezi mepesi, ambapo anaamini wengi wao watakuwepo katika mchezo huo.
    Alisema wachezaji wengi wote wanaendelea vizuri na mazoezi chini yao, na kuwa wamejipanga kuhakikisha kikosi chao kinashinda katika mchezo huo.
    Yanga inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu, baada ya kufikisha pointi 46, sawa na Azam, lakini wanapishana kwa tofauti ya magoli, imeweka kambi visiwani Pemba, kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Azam FC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWAMBUSI: AZAM WAGUMU, LAKINI 'TUTAWANYOROSHA' TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top