• HABARI MPYA

  Friday, March 11, 2016

  LIVERPOOL YAILAZA 2-0 MAN UNITED, SPURS YACHEZEA 3-0 KWA BORRUSIA DORTMUND

  MATOKEO MECHI ZA KWANZA 16 BORA UEFA EUROPA LEAGUE
  Machi 10, 2016  
  Sparta Prague 1-1 Lazio
  Athletic Club 1-0 Valencia CF
  Liverpool 2-0 Manchester United
  Villarreal 2-0 Bayer 04 Leverkusen
  FC Basel 0-0 Sevilla
  Borussia Dortmund 3-0 Tottenham Hotspur
  Fenerbahce 1-0 Sporting Braga
  Shakhtar Donetsk 3-1 RSC Anderlecht
  Mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino akikimbia kushangilia baada ya kuifungia timu yake bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Manchester United usiku huu Uwanja wa Anfield PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  LIVERPOOL imejiweka katika nafasi nzuri ya kwenda Robo Fainali ya michuano ya UEFA Europa League, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mahasimu wao, Manchester United Uwanja wa Anfield usiku wa Alhamisi.
  United sasa watatakiwa kwenda kushinda 3-0 katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Machi 17 Uwanja wa Old Trafford ili kwenda Robo Fainali.
  Katika mchezo huo, bao la kwanza la Liverpool lilifungwa na Daniel Sturridge kwa penalti dakika ya 20, baada ya Nathaniel Clyne kuangushwa na Memphis Depay kwenye boksi.
  Mshambuliaji Mbrazil, Roberto Firmino Barbosa de Oliveira akaongeza matumaini ya Liverpool kwenda Robo Fainali baada ya kufunga bao la pili dakika ya 73.
  Mchezo mwingine, Borussia Dortmund imeanza vyema kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Tottenham Hotspur ya England mabao ya Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 30 na Marco Reus dakika ya 61 na 70 Uwanja wa Signal Iduna Park mjini Dortmund, Ujerumani.
  Sparta Prague imelazimishwa sare ya 1-1 na Lazio Uwanja wa Jenerali, bao lao likifungwa na Martin Frydek dakika ya 13, kabla ya Marco Parolo kuwasawazishia wageni dakika ya 38, wakati Athletic Club imeshinda 1-0 dhidi ya Valencia CF, bao pekee la Raul Garcia Escudero dakika ya 20 Uwanja wa San Mames.
  Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre Aubameyang akipongezana na mchezaji mwenzake, Marco Reus baada ya wote kufunga katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Tottenham PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Villarreal imeshinda 2-0 dhidi ya Bayer 04 Leverkusen, mabao ya Cedric Bakambu dakika ya nne na 56 Uwanja wa El Madrigal, wakati FC Basel imetoka sare ya 0-0 na Sevilla Uwanja wa St Jakob-Park.
  Fenerbahce imeshinda 1-0 dhidi ya Sporting Braga, bao pekee la Mehmet Topal dakika ya 82 Uwanja wa Ulker Stadyumu, wakati Shakhtar Donetsk imeichapa 3-1 RSC Anderlecht, mabao yake yakifungwa na Taison Barcellos Freda dakika ya 21, Olexandr Kucher dakika ya 24 na Eduardo Alves da Silva dakika ya 79, huku la wageni likifungwa na Frank Acheampong dakika ya 68 Uwanja wa Lviv.
  Mechi zote za marudiano zitafanyika Machi 17 na washindi wa jumla watakwenda Robo Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAILAZA 2-0 MAN UNITED, SPURS YACHEZEA 3-0 KWA BORRUSIA DORTMUND Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top