• HABARI MPYA

    Monday, March 14, 2016

    ESPERANCE YABISHA HODI AZAM FC

    MATOKEO MECHI ZA KWANZA RAUNDI YA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
    Ijumaa, Machi 11, 2016
    UMS Loum (Cameroon) 1-1 FUS Rabat (Morocco)
    Jumamosi, Machi 12, 2016
    V. Club Mokanda (Kongo) 0-0 Police (Rwanda)
    Sagrada Esperanca (Angola) 1-0 Liga Desportiva (Msumbiji)
    MC Oran (Algeria) 2-0 SC Gagnoa (Ivory Coast)
    Kawkab Athletic (Morocco) 3-0 BYC (Liberia)
    Bidvest (Afrika Kusini) 0-3 Azam (Tanzania)
    Renaissance (Chad) 0-2 Esperance (Tunisia)
    Harare City (Zimbabwe) 1-2 Zanaco (Zambia)
    Stade Gabesien (Tunisia) 2-1 AS Kaloum (Guinea)
    Misr Makkassa (Misri) 3-1 Don Bosco (DRC)
    Athletico (Burundi) 0-2 Mounana (Gabon)
    Africa Sports (Ivory Coast) 0-2 ENPPI (Misri)
    Jumapili Machi 13, 2016
    Nasarawa United FC (Nigeria) 1-0 Club Sportif Constantinois (Ageria)
    FC Saint Eloi Lupopo (DRC)  2-1 El Ahly Shandy (Sudan)
    Al Ittihad (Libya)  1-0 Medeama (Ghana)
    Azam FC inaweza kukutana na Esperance ya Tunisia mwezi ujao katika Kombe la Shirikisho  

    MECHI kati ya Azam FC na Esperance ya Tunisia ipo njiani. Hiyo inafuatia timu zote kushinda mechi zao za kwanza ugenini za Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika mwishoni mwa wiki.
    Wakati Azam FC iliaadhibu Bidvest Wits mabao 3-0 mjini Johannesburg, Afrika Kusini Jumamosi, Esperance iliichapa mabao 2-0 Renaissance nchini Chad siku hiyo hiyo.
    Na hii itakuwa mara ya kwanza kabisa kwa Azam FC kwa ujumla kwenda kucheza Tunisia, ingawa si mara ya kwanza kucheza nchi za Kaskazini mwa Afrika, wakati Esperance si wageni Tanzania, kwani wamekwishakuja mara kadhaa.
    Mara ya mwisho Esperance iliitoa Yanga SC katika Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2007 kwa jumla ya mabao 3-0, iliyoshinda mjini Tunis kabla ya kutoa sare ya 0-0 mjini Mwanza.
    Mwaka 2013 Azam FC ilitolewa na FAR Rabat ya Morocco baada ya sare ya 0-0 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 2-1 mjini Rabat.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ESPERANCE YABISHA HODI AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top