• HABARI MPYA

    Thursday, October 08, 2015

    MWAMBUSI KURITHI MIKOBA YA MKWASA YANGA SC, MAMBO MATATU YAMPA ULAJI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    YANGA SC ipo kwenye mazungumzo na kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi (pichani kulia) akachukue nafasi ya Charles Boniface Mkwasa aliyekuwa Msaidizi wa Mholanzi, Hans van der Pluijm.
    Mkwasa amesaini Mkataba wa mwaka mmoja na nusu kufundisha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na tayari ameaga Yanga SC.
    Kwa sababu hiyo, mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wanataka mbadala wa Mkwasa haraka iwezekanavyo na rada zao zimemlenga Mwambusi.
    BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE inafahamu baada ya mchakato wa kupitia majina kadhaa yaliyopendekezwa, jina la Mwambusi lilipita bila ya kipingamizi hususan kutokana na kupendekezwa pia kocha Mkuu, Pluijm.
    Mambo matatu yamempa nafasi Mwambusi Yanga SC, ni muadilifu, mchapakazi na hana majungu.
    “Mwambusi ni mtu wa ibada, hana majungu, anaweza kuishi na wachezaji wa aina yoyote. Ana nidhamu na kwa ujumla ana haiba nzuri,”kimesema chanzo kutoka Yanga SC.
    Mwambusi yuko Dar es Salaam tangu juzi kwa mazungumzo na Yanga SC ingawa haijulikani Mkataba wake ukoje Mbeya City.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWAMBUSI KURITHI MIKOBA YA MKWASA YANGA SC, MAMBO MATATU YAMPA ULAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top