• HABARI MPYA

    Thursday, November 14, 2019

    MOROCCO AITA WACHEZAJI 40 KIKOSI CHA AWALI CHA ZANZIBAR HEROES KOMBE LA CHALLENGE

    Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
    KOCHA wa timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Hemed Suleiman ‘Morocco’ ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 40 kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge inayotarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 1 hadi 19 nchini Uganda.
    Morocco amesema kwamba wachezaji hao 40 wakiwemo wanne wa klabu ya Yanga SC wataingia kambini kwa maandalizi ya awali na baadaye watachujwa na kubaki 23 ambao ndio watakwenda Uganda kwenye michuano hiyo.
    Kikosi hicho kinaundwa na makipa; Abdulatif Said Masoud (Jamhuri), Mohamed Abrahman (JKT Tanznaia), Mohamed Muali (Polisi Tanzania), Abdallah Rashid ‘Babu’ (Ruvu Shooting), Haji Juma ‘Chafu’ (JKU) na Ahmed Ali ‘Salula’ (Malindi).

    Mabeki ni Suleiman Said Juma (Zimamoto), Mohammed Othman Mmanga (Polisi Tanzania), Ibrahim Mohamed ‘Sangula’ (KVZ), Mwinyi Haji Mngwali (KMKM), Juma Kukuti Adam (Polisi Tanzania), Ally Haji (Mwenge), Abdul Malik Adam (Mafunzo), Ali Juma Maarifa (Malindi), Issa Haidar Dau (JKU), Abdallah Kheri (Azam), Ibrahim Ame Mohd (Coastal Union), Ally Ally (Yanga), Abubakar Ali (Mlandege), Ibrahim Hamad (Malindi), Aggrey Morris (Azam) na Abubakar Ame ‘Luiz’ (Malindi).
    Viungo ni Abdul aziz Makame (Yanga), Abdul Swamad Kassim (Kagera Sugar), Awesu Awesu (Kagera Sugar), Mudathir Yahya (Azam), Isihaka Said (KMKM), Adam Ibrahim ‘Edo’ (KMKM), Kassim Suleiman (Azam), Haroun Abdallah (Zimamoto), Feisal Salum (Yanga), Mohamed Issa (Yanga), Mustafa Muhsin ‘Park’ (Zimamoto), Helefin Salum (Mlandege), Baraka Shaaban (Ruvu Shooting), Khalid Shaaban (Rich Boys), Abdallah Hassan Nassor ‘Abal’ (Polisi Tanzania), Mohamed Mussa (Mbeya City), Mohamed Abdallah (Mlandege) na Ally Juma ‘Larson’ (Mafunzo).
    Washambuliaji ni Ibrahim Hamad ‘Hilika’ (Zimamoto), Abdulnasir Asaa (Mlandege), Khamis Mussa ‘Rais’ (Malindi), Said Salum ‘Eto’o’ (Kipanga), Ibrahim Abdallah ‘Imu Mkoko’ (Malindi) na Mussa Ali Mbarouk (KMKM).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOROCCO AITA WACHEZAJI 40 KIKOSI CHA AWALI CHA ZANZIBAR HEROES KOMBE LA CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top