• HABARI MPYA

  Monday, March 11, 2019

  NINJA WA YANGA AFUNGIWA MECHI TATU KWA KUMPIGA KIWIKO MCHEZAJI WA COASTAL UNON

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungia mechi tatu beki wa Yanga SC, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union  katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Taarifa ya Afisa Habari Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo kwa Vyombo vya Habari leo imesema kwamba uamuzi huo umechukuliwa katika kikao cha Kamati hiyo jana Jumapili Machi 10, 2019 na kupitia mashauri mbalimbali yaliyofikishwa kwenye Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Wakili Kiomoni Kibamba.
  Ndimbo amesema kwamba Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo/zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1)(d) cha Kanuni za Nidhamu TFF ingawa ana Haki ya kukata rufaa.

  Daktari Samwel Peter amelalamikiwa mbele ya kamati ya nidhamu kuwa Februari 02 2019 kati ya timu yake na Rhino Rangers alifanya vitendo vya utovu wa nidhamu. Kamati imemtia hatiani Samwel Peter kwa kosa la kufanya vitendo  vya utovu wa nidhamu.
  Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kujihusisha na mpira wa miguu kwa muda wa miezi mitatu na faini ya Tsh laki tano (500,000/=) kwa mujibu wa kanuni ya 41(7) kanuni za Ligi Daraja la Kwanza, ingawa ana Haki ya kukata rufaa iko wazi, adhabu zote zinakwenda kwa pamoja.
  Kocha wa makipa wa Arusha United SC, Mfaume Ally amelalamikiwa mbele ya kamati ya nidhamu kuwa Februari 02 2019 kati ya timu yake na Rhino Rangers alifanya vitendo vya utovu wa nidhamu
  Na baada ya mlalamikiwa kutokuwepo bila taarifa, Kamati imemtia hatiani Mfaume Ally kwa kosa la kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu na kumfungia michezo mitatu (3) na faini ya Tsh laki tano (300,000/=) kwa mujibu wa kanuni ya 40(1) kanuni za Ligi Daraja la Kwanza, ingawa ana Haki ya kukata rufaa.
  Daktari wa Biashara United Laurent Kimaro amelalamikiwa mbele ya kamati ya nidhamu kuwa Janaruari 25 2019 alitolewa kwenye benchi kwa kosa la kupinga maamuzi ya mwamuzi kati ya timu yake na Azam Fc.
  Mlalamikiwa alituma utetezi wa maandishi na kukana kufanyika kwa kitendo hicho na baada ya mlalamikaji kushindwa kuthibitishwa kosa, kamati imetupilia mbali malalamiko hayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NINJA WA YANGA AFUNGIWA MECHI TATU KWA KUMPIGA KIWIKO MCHEZAJI WA COASTAL UNON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top