• HABARI MPYA

  Monday, March 11, 2019

  MCHEZAJI WA ALLIANCE ALIYEMTOMASA MAKALIO GARDIEL MICHAEL AFUNGIWA MECHI TATU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZAJI wa Alliance FC ya Mwanza, Juma Nyangi amefungiwa mechi tatu na faini ya Sh. Milioni 2 kwa kitendo cha kumtomasa makalio beki wa Yanga, Gardiel Michael.
  Kipa Benedict Mlekwa Tinoco amelalamikiwa mbele ya kamati ya nidhamu kuwa Februari 14 2019 kati ya timu yake ya Mtibwa Sugar na Biashara United Fc alimkanyaga kwa makusudi mchezaji wa timu pinzani aliyekuwa ameanguka baada ya kuchezewa rafu
  Mlalamikiwa aliwakilishwa na kiongozi wa Timu yake, Ndg. Swabura Abubakar, mwakilishi wa mlalamikiwa alikiri kosa na kuomba msamaha.
  Kamati imemtia hatiani Benedict Mlekwa Tinoco kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa timu pinzani aliyekuwa ameanguka baada ya kuchezewa rafu
  Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo/zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1)(d) cha Kanuni za Nidhamu TFF ingawa ana Haki ya kukata rufaa.
  Meneja wa  Transiti Camp, John Mchemba amelalamikiwa Kamati ya Nidhamu kuwa tarehe 10/11/2018 katika mechi namba 31, kundi B dhidi ya Green Warriors iliyofanyika Azam Complex alianzisha vurugu na kusababisha mchezo kusimamishwa. Baadae alipelekwa jukwaa kuu lakini aliendelea na vurugu hizo.
  Na baada ya mlalamikiwa kutokuwepo bila taarifa, Kamati baada ya kupitia ripoti zote, imetoa adhabu ya kufungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2)ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, faini  ilipwe ndani ya siku 30.
  Meneja wa Polisi Tanzania, Nelson William amelalamikiwa Kamati ya Nidhamu kuwa tarehe 19/01/2019 katika mechi namba 63, kati ya timu yake na Boma Fc alipigana na washabiki.
  Na baada ya mlalamikiwa kutokuwepo bila taarifa, Kamati imemtia hatiani Nelson William kwa kosa la kupigana na washabiki na kumfungia kujihusisha na mpira wa miguu kwa muda wa miezi sita na faini ya Tsh laki nne (400,000/=) kwa mujibu wa kifungu cha 41(2) cha kanuni za ligi daraja la kwanza.
  Vile vile kamati imetoa adhabu kwa timu ( Polisi Tanzania ) faini ya Tsh laki tano ( 500,000/=) kwa mujibu wa kanuni ya 15(2) kanuni za nidhamu za TFF,kwa kosa la kuendela kumtumia kiongozi ambaye amefungiwa kujihusisha na mpira wa miguu.
  Kamati imeagiza bodi ya uendeshaji wa ligi, kuwa kama meneja tajwa hapo juu ataendelea kutumika basi timu ifutiwe matokeo kwa kila mchezo watakaomtumia, adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 12(e) ya kanuni za nidhamu TFF.
  Mchezaji wa Polisi Tanzania, Green Paul amelalamikiwa Kamati ya Nidhamu kuwa tarehe 19/01/2019 katika mechi namba 63, kati ya timu yake na Boma Fc alimpiga mwamuzi msaidizi.
  Na baada ya mlalamikiwa kutokuwepo bila taarifa, Kamati haikujiridhisha na utetezi wa mlalamikaji ivyo basi imetoa onyo kwa malalamikiwa kwa mujibu wa kifungu cha kanuni za nidhamu za TFF.
  Meneja wa Kasulu Red Star FC, Mfungo Bita amelalamikiwa Kamati ya Nidhamu kuwa tarehe 17/11/2018 alifanya vitendo vya utovu mkubwa wa nidhamu kwenye mechi dhidi ya Bulyanhulu FC na  Kasulu Red Star.
  Na baada ya mlalamikiwa kutokuwepo bila taarifa, Kamati imemtia hatiani Mfungo Bita kwa kosa la kufanya vitendo  vya utovu wa nidhamu.
  Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutojihusisha na mpira wa miguu kwa muda wa miezi mitatu na faini ya Tsh laki tano (500,000/=) kwa mujibu wa kanuni ya 41(7) kanuni za Ligi Daraja la Pili ingawa Haki ya kukata rufaa iko wazi, adhabu zote zinakwenda kwa pamoja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHEZAJI WA ALLIANCE ALIYEMTOMASA MAKALIO GARDIEL MICHAEL AFUNGIWA MECHI TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top