• HABARI MPYA

    Thursday, March 28, 2019

    SERENGETI BOYS YATUA KIGALI KUSHIRIKI MICHUANO MAALUM KUJIANDAA NA AFCON U17

    Na Mwandishi Wetu, KIGALI
    KIKOSI cha timu ya taifa ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kimewasili salama mjini Kigali nchini Rwanda kushiriki mashindano maalum ya maandalizi ya fainali za U17 Afrika, (AFCON U17 2019).
    Tanzania itakuwa mwenyeji wa AFCON (U17 mwezi ujao na katika kujiandaa na fainali hizo wamekwenda kushiriki mashindano hayo maalum ya mataifa matatu, mengine yakiwa ni Cameroon na wenyeji Rwanda.
    Kikosi cha Serengeti Boys kilichowasili mjini Kigali leo kinaundwa na Mwinyi Abdallah, Shaaban Hassan, Zubeiry Foba, Pascal Gaudence, Ally Hamisi, Ben Anthony, Mohamed Omary, Dominic Pauline, Mustapha Rashid na Maurice Michael.
    Wengine ni Agiri Aristide, Edson Jeremiah, Tepsi Evance, Charles Herman, Kelvin Pius, Edmund Godfrey, Salum Ally, Arafat Hussein, Misungwi Boniface, Ladaki Juma, Jefferson Mwaikambo, Benard Castory na Omary Jumanne.
    Na Serengeti Boys inakwenda Kigali kushiriki michuano hiyo wiki tatu tangu irejee kutoka Uturuki ilipokwenda kushiriki michuano ya UEFA Assist ambako ilishinda mechi moja 3-2 dhidi ya Australia na kufungwa mbili, 1-0 na Guinea na 5-0 na wenyeji, Uturuki Uwanja wa Emirhan Sports Complex mjini Antalya.
    Wakati huo huo: Kikosi cha timu ya taifa ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes kikiwa na jumla ya wacheza 20 na viongozi wanane, kimekwenda mjini Asmara Eritrea ambako Jumapili watacheza mchezo wa kirafiki na wenyeji wao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS YATUA KIGALI KUSHIRIKI MICHUANO MAALUM KUJIANDAA NA AFCON U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top