• HABARI MPYA

  Monday, March 11, 2019

  ISACK GAMBA AFUNGIWA KWA KUWATUKANA MAREFA IHEFU IKIICHAPA KITAYOSCE 2-1 MBEYA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Isack Gamba wa Kitayosce FC, amefungiwa mechi mbili na kutozwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya kuondolewa kwenye benchi la ufundi kwa kosa la kutoa lugha chafu kwa waamuzi katika mechi namba 29 ya Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara dhidi ya Ihefu FC  Januari 12, 2019 Uwanja wa Highland Estate, Mbeya.
  Taarifa ya Afisa Habari Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo kwa Vyombo vya Habari leo imesema kwamba, katika mchezo huo ambao Ihefu FC ilishinda 2-1, adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 41(11) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Udhibiti kwa Makocha.
  Mechi namba 32- Usalama FC 1 vs The Might Elephant FC 1; Daktari wa The Might Elephant, Shaaban Sengo amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la kuingilia ugomvi kati ya washabiki wa timu yake dhidi ya wale wa Usalama FC kwenye mchezo huo uliofanyika Januari 12, 2019 kwenye Uwanja wa Singe Sekondari mjini Babati.

  Mechi namba 29- Kasulu Red Star FC 0 vs Area C United 0; Kipa wa akiba wa Area C United, Abdul Mohamed amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la kumpiga Kamishna na kutoa lugha ya matusi katika mchezo huo uliofanyika Januari 12, 2019 Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Mechi namba 37- Kumuyange FC 2 vs Kasulu Red Star FC 2; Mchezaji wa Kasulu Red Star, Timotheo T. Gugamwa amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la kujaribu kumpiga Mwamuzi katika mchezo huo uliofanyika Februari 2, 2019 Uwanja wa Kabanga Sekondari ulioko Ngara, Kagera.
  Mechi namba 45- Toto Africans 2 vs Milambo FC 1; Klabu ya Milambo FC imepewa Karipio Kali baada ya kuchelewa kufika uwanjani kwa nusu saa katika mchezo huo uliofanyika Februari 17, 2019 Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo.
  Mechi namba 48- Area C United 0 vs Kumuyange FC 0; Klabu ya Kumuyange FC imetozwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kutokana na timu yake kutohudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) kwa ajili ya mchezo huo uliofanyika Februari 17, 2019 Uwanja wa Kibaigwa, Dodoma. 
  Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo. Naye Meneja wa Kumuyange FC, Joseph Sinzo amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya kumwaga maji kwenye chumba cha kubadilishia cha timu ya Area C United.
  Mechi namba 32- African Sports 1 vs Changanyikeni Rangers FC 0. 
  Kamishna Beda Lyimo na Mwamuzi Sebastian Sanga wamepewa Onyo kutokana na ripoti zao kuwa na upungufu katika mchezo huo uliofanyika Januari 15, 2019 Uwanja wa Nyamagana
  jijini Mwanza. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Daraja la Pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ISACK GAMBA AFUNGIWA KWA KUWATUKANA MAREFA IHEFU IKIICHAPA KITAYOSCE 2-1 MBEYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top