• HABARI MPYA

  Monday, March 11, 2019

  TIMU 28 ZAGAWANYWA KATIKA MAKUNDI MANNE KUCHEZA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) itachezwa katika vituo vinne katika Mikoa ya Tanzania Bara, ikianza Machi 27, 2019 na kumalizika April 11, 2019 katika hatua ya Makundi.
  Taarifa ya Afisa Habari Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo kwa Vyombo vya Habari leo imesema kwamba, timu mbili (2) za juu kutoka katika kila kundi zitafuzu kucheza hatua ya Nane (8) Bora katika kituo kimoja kitakachotangazwa na TFF.
  Hatua ya nane Bora itakua na makundi mawili (2) yenye timu nne kwa kila kundi, ambapo timu mbili za juu zitafuzu hatua ya Nusu Fainali na hatimae Fainali.
  Ndimbo amesema washindi watatu (3) watapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Pili msimu wa 2019/2020.
  Amevitaja Vituo vya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) 2018/2019 ni: SIMIYU - Uwanja wa Halmashauri Bariadi, KATAVI - Uwanja wa Azimio Mpanda, SONGWE - Uwanja wa Viwawa Mbozi na DODOMA - Uwanja wa Mgambo Mpwapwa.
  KUNDI A litakuwa kituo cha SIMIYU likiundwa na timu za Bariadi United (Simiyu), Copco Veteran (Mwanza), Hawita (Mara), Mbuni FC (Arusha), Red Star (Manyara), Buyuni FC (Dar es salaam), Ujenzi FC (Shinyanga).
  KUNDI B – KATAVI: Mkurugenzi FC (Katavi), Mpui FC (Rukwa), Sabasaba FC (Tabora), Tallinega FC (Kigoma), Isanga Rangers (Mbeya), Masumbwe FC (Geita), Umoja Chandimu (Kagera).
  KUNDI C – SONGWE: Mpira Pesa FC (Songwe), Deportivo Mang’ula (Morogoro), Makete United (Njombe), Coastal Star (Pwani), Nzihi FC (Iringa), Top Boys (Ruvuma), DTB FC (Dar es salaam).
  KUNDI D – DODOMA: Mji Mpwapwa FC(Dodoma), Pan African (Dar es salaam), Stand Misuna (Singida), Majengo United (Tanga), New Generation (Kilimanjaro), Timberland FC (Lindi), Tandahimba FC (Mtwara).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU 28 ZAGAWANYWA KATIKA MAKUNDI MANNE KUCHEZA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top