• HABARI MPYA

  Monday, April 16, 2018

  ZANZIBAR WAFUNGIWA KUSHIRIKI CECAFA U-17 KWA KUPELEKA WAKUBWA, SERENGETI YATOA SARE NA BURUNDI

  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Zanzibar, Karume Boys imefungiwa mwaka mmoja kushiriki michuano ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Cup U17 na kupigwa faini ya dola za Kimarekani 15,000 kwa kosa la kupeleka wachezaji waliozidi umri.
  Michuano ya CECAFA Challenge Cup U17 inaendelea nchini Burundi na Zanzibar inadaiwa kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya Januari 1 mwaka 2002, ambao wazi wamezidi umri unaotakiwa wa miaka 17.
  Jana timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania Bara, Serengeti Boys ilitoa sare ya 1-1 na Uganda katika mechi yake kwanza ya michuano hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZANZIBAR WAFUNGIWA KUSHIRIKI CECAFA U-17 KWA KUPELEKA WAKUBWA, SERENGETI YATOA SARE NA BURUNDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top