• HABARI MPYA

  Friday, April 06, 2018

  WAMBURA AGONGA MWAMBA KAMATI YA RUFAA YA TFF, ADHABU IPO PALE PALE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa shirikisho hilo, Michael Richard Wambura aliyepinga kufungiwa maisha.
  Wambura alifungiwa maisha na Kamati ya Maadili kufuatia mashitaka aliyofungiwa na Sekretarieti ya TFF.
  Mwenyekiti wa kamati ya Rufani, Ebenezer Mshana, amewaambia Waandishi wa Habari leo kwamba baada ya kusikiliza na kuchanganua hoja za pande zote mbili, waliona kwamba Wambura amekutwa na hatia.
  Rufaa ya Michael Wambura (kulia) imetupiliwa mbali na sasa ataendelea kutumikia kifungo cha maisha kutojihusisha na soka

  "Baada ya kuzisikiliza rufani zote za Wambura, tumeona kwamba Wambura alikuwa na makosa, hivyo tunaiomba sekretarieti ya TFF iende mbali zaidi katika kesi hii," alisema.
  Naye wakili wa Wambura, Emmanuel Muga, alisema mteja wake alikwishajua kwamba hicho ndicho kitu kitakachotokea baada ya Kamati kubadilishwa.
  "Wambura aliniambia kwamba mkutano ukimaliza niongee na nyinyi kwa sababu alikwishajua kitu ambacho kitatokea, lakini tutakata rufaa na kwenda mbele," alisema.
  Muga aliongeza kwamba alishangazwa na Mwenyekiti huyo kusoma upande wa TFF, kwamba aliomba mteja wake apunguziwe adhabu na iwe miaka mitano badala ya kufungiwa maisha.
  "Kama ningekuwa nimesema hivyo, basi ingesomwa katika utetezi wetu, lakini haikusemwa ni jambo ambalo linashtua, tutakata rufaa na kwenda mbele zaidi," alisema.
  Rufaa zingine zilizosomwa na Ebenezer, rufani ya Edgar Chibula kiongozi wa Abajalo, ambaye alitoa maneno machafu baada ya kuhairishwa mchezo wao dhidi ya Prison, lakini aliomba msamaha katika kamati na kukiri hivyo amesemahewa.
  Rufani nyingine ni ya kiongozi wa Ndanda, Dunstan Mkundi ambaye kesi yake kamati imeamuru Tff kupeleka suala lake kwenye vyombo vya uchunguzi.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAMBURA AGONGA MWAMBA KAMATI YA RUFAA YA TFF, ADHABU IPO PALE PALE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top