• HABARI MPYA

    Tuesday, April 10, 2018

    LWANDAMINA ‘ATOROKA’ YANGA SC YADAIWA AMEREJEA ZESCO UNITED…JANGWANI WAHAHA KUMSAKA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mzambia, George Lwandamina ameondoka leo kwenda Zambia na habari zinasema anarejea Zesco United ya kwao na atatambulishwa Alhamisi.
    Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Lwandamina hajatokea mazoezini leo asubuhi bila sababu na wanamtafuta hapatikani.
    “Mimi sijui kaenda wapi, kwa sababu hajaniaga. Hizo habari (za kwenda Zambia) wewe ndiyo unaniambia,”amesema Mkwasa baada ya kuulizwa na Bin Zubeiry Sports – Online juu ya kocha huyo kurejea kwao, Zambia.
    George Lwandamina ameondoka leo kwenda Zambia na habari zinasema anarejea Zesco United ya kwao

    Habari zinasema kwamba Zesco United imeamua kumrejesha kocha wake huyo baada ya mafanikio yake Tanzania ndani ya miaka miwili, akiiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita na sasa inakaribia kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
    Yanga SC imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolaita Ditcha ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua hiyo Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ushindi huo uliotokana na mabao ya Raphael Daudi kipindi cha kwanza na Emmanuel Martin kipindi cha pili, unamaanisha Yanga SC watahitaji kwenda kulazimisha sare ugenini wiki ijayo, au kutofungwa zaidi ya tofauti ya bao moja ili kwenda hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya pili baada ya mwaka 2016.
    Na Lwandamina ambaye mkataba wake unamalizika Juni mwaka huu, anaondoka Yanga siku moja kabla ya kuteremka uwanjani kumenyana na Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Lwandamina alijiunga na Yanga Novemba mwaka 2016 akichukua nafasi ya Mholanzi, Hans van der Pluijm na katika kipindi hicho ameiongoza timu katika michezo 77 ya mashindano yote akitoa sare 18, kushinda 45 kati ya hizo mbili kwa penalti baada ya sare ndani ya muda wa kawaida na kufungwa 14, tano kwa penalti baada ya sare katika muda wa kawaida.

    George Lwandamina wakati anatambulishwa Yanga Novemba 25 mwaka 2016 kichukua nafasi ya Mholanzi, Hans van der Pluijm 

    REKODI YA LWANDAMINA YANGA SC
    Mechi 77 | kushinda 45 | sare 18 | kufungwa 14   
    Yanga SC 0-2 JKU (Kirafiki Uhuru)
    Yanga SC 2-0 JKT Ruvu (Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga SC 1-1 African Lyon (Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga SC 4-0 Ndanda FC (Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 6-0 Jamhuri (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga 2-0 Zimamoto (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga 0-4 Azam (Kombe la Mapinduzi)
    Yanga 0-0 Simba (Penalti 2-4 Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Yanga 1-0 Maji Maji (Ligi Kuu Songea)
    Yanga 4-1 Ashanti United (Kombe la TFF, Uhuru)
    Yanga 2-0 Mwadui FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 4-0 Stand United (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 5-1 Ngaya de Mde (Ligi ya Mabingwa Moroni)
    Yanga 1-1 Ngaya de Mde (Ligi ya Mabingwa Taifa)
    Yanga 1-2 Simba (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 2-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 0-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Jamhuri)
    Yanga 0-0 Kiluvya United (Kombe la TFF Uhuru)
    Yanga 1-1 Zanaco (Ligi ya Mabingwa Taifa)
    Yanga 0-0 Zanaco (Ligi ya Mabingwa Lusaka)
    Yanga 1-0 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 1-0 MC Alger (Mchujo wa kufuzu Makundi Kombe la Shirikisho, Taifa)
    Yanga 0-4 MC Alger (Mchujo wa kufuzu Makundi Kombe la Shirikisho, Algiers)
    Yanga 3-0 Prisons (Robo Fainali Kombe la TFF Taifa)
    Yanga 0-1 Mbao FC (Nusu Fainali Kombe la TFF Mwanza)
    Yanga 2-0 Tanzania Prisons (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 2-1 Mbeya City (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 1-0 Toto Africans (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 0-1Mbao FC (Ligi Kuu Kirumba)
    Yanga 3-0 AFC (Alibaki Dar, kirafiki Arusha)
    Yanga 0-0 (Pen 4-2) Tusker FC (SportPesa Super Cup, alikuwa likizo Zambia)
    Yanga 0-0 (Pen 2-4) AFC Leopards (SportPesa Super Cup, alikuwa likizo Zambia)
    Yanga 3-2 Singida United (Kirafiki Taifa)
    Yanga 0-1 Ruvu Shooting (Kirafiki - Chamazi)
    Yanga 2-0 Mlandege (Kirafiki Zanzibar)
    Yanga 1-0 Chipukizi (Kirafiki Pemba)
    Yanga 0-0 (4-5 penalti) Simba (Ngao ya Jamii, Taifa)
    Yanga 1 – 1 Lipuli (Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 0-0 KMC (Kirafiki Chamazi)
    Yanga 1-0 Njombe Mji (Ligi Kuu Saba Saba, Njombe)
    Yanga 1-1 Maji Maji (Ligi Kuu Maji Maji, Songea)
    Yanga 1-0 Ndanda (Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 0-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu Bukoba)
    Yanga 0-0 Rhino Rangers (Kirafiki A. Mwinyi, Tabora)
    Yanga SC 4-0 Stand United (Ligi Kuu Kambarage, Shinyanga)
    Yanga 1-1 Simba (Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 0-0 Singida United (Ligi Kuu Namfua, Singida)
    Yanga 5-0 Mbeya City (Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 1-1 Tanzania Prisons (Ligi Kuu Chamazi)
    Yanga SC 2-0 Reha FC (Alikuwa Zambia msiba wa mwanawe 64 Bora Kombe la TFF Uhuru)
    Yanga SC 0-2 Mbao FC (Alikuwa Zambia msiba wa mwanawe Ligi Kuu Kirumba)
    Yanga 2-1 Mlandege (Alikuwa Zambia msiba wa mwanawe Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga SC 1-0 JKU (Alikuwa Zambia msiba wa mwanawe Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga SC 2-0 Taifa Jang’ombe (Alikuwa Zambia msiba wa mwanawe Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga SC 1-0 Zimamoto (Alikuwa Zambia msiba wa mwanawe Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga SC 1-1 Singida United (Alikuwa Zambia msiba wa mwanawe Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga SC 0-0 (pen4-5) URA (Alikuwa jukwaani sababu ya kibali Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga 0-0 Mwadui FCi (Alikuwa jukwaani sababu ya kibali Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 1-0 Ruvu Shooting  (Alikuwa jukwaani sababu ya kibali Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 2-1 Azam FC  (Ligi Kuu Chamazi)
    Yanga 1-1 (pen4-3) Ihefu FC  (Kombe la TFF Sokoine, Mbeya)
    Yanga 2-0 Lipuli FC  (Ligi Kuu, Samora, Iringa)
    Yanga 4-0 Njombe Mji FC  (Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 1-0 Saint Louis FC  (Ligi ya Mabingwa, Taifa)
    Yanga 4-1 Maji Maji FC  (Ligi Kuu, Taifa)
    Yanga 1-1 Saint Louis FC  (Ligi ya Mabingwa, Mahe)
    Yanga 2-1 Maji Maji FC  (Kombe la TFF Maji Maji, Songea)
    Yanga 4-1 Maji Maji FC  (Ligi Kuu, Taifa)
    Yanga 2-1 Ndanda FC  (Ligi Kuu, Nangwanda)
    Yanga 1-2 Township Rollers  (Ligi ya Mabingwa Taifa)
    Yanga 3-0 Kagera Sugar (Ligi Kuu, Taifa)
    Yanga 3-1 Stand United (Ligi Kuu, Taifa)
    Yanga 0-0 Township Rollers  (Ligi ya Mabingwa Gaborone)
    Yanga 1-1 (Penalti 2-4) Singida United (Kombe la TFF Maji Maji, Namfua)
    Yanga 2-0 Wolaita Ditcha  (Kombe la Shirikisho Dar es Salaam)  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LWANDAMINA ‘ATOROKA’ YANGA SC YADAIWA AMEREJEA ZESCO UNITED…JANGWANI WAHAHA KUMSAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top