• HABARI MPYA

    Monday, January 15, 2018

    WAMBURA, MGOYI NA WENGINE WAWILI TFF WAPEWA UKAMISAA CAF

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limepitisha majina manne ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa Makamisaa wa michezo mbalimbali inayoandaliwa na bodi ya mchezo barani. 
    Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizotoa Makamisaa wanne ambayo ni idadi ya juu hakuna nchi iliyozidisha idadi hiyo ambayo ni kwa kipindi cha kutokea mwaka 2018 mpaka 2020.
    Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF waliopata nafasi hiyo ni Makamu wa Rais Michael Wambura, Ahmed Mgoyi, Amina Karuma na Sarah Tchao.
    Wambura kwa upande wake amechaguliwa kutokana na kufanya vizuri katika aiku za nyuma wakati Mgoyi amepata nafasi hiyo kwa kufanya vizuri kama mechi kamishna wa michezo ya CECAFA nao Karuma na Tchao wameipata nafasi hiyo kutokana na  mkakati wa CAF kuanza kuwajengea uwezo viongozi wanawake vijana.
    Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura (kulia) akiwa na Rais wake, Wallace Karia

    Kuteuliwa kwa viongozi hao wa TFF ni muendelezo CAF kuteua viongozi wa TFF kwenye kamati mbalimbali itakumbukwa hivi karibuni Rais wa TFF aliteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya fainali za Africa kwa wachezaji wa ndani CHAN inayoendelea nchini Morocco lakini pia akiteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya ufunguzi iliyowakutanisha wenyeji Morocco na Mauritania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAMBURA, MGOYI NA WENGINE WAWILI TFF WAPEWA UKAMISAA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top