• HABARI MPYA

  Monday, January 15, 2018

  TISA WACHUJWA SERENGETI BOYS, KAMBINI KUVUNJWA JANUARI 28

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WACHEZAJI tisa wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys wamepunguzwa kwenye kikosi cha timu hiyo kinachoendelea na maandalizi ya michuano mbalimbali.
  Kikosi sasa kinabaki na wachezaji 34 kutoka 43 na kiitaendelea kuwepo kambini hadi Januari 28, 2018. Orodha hiyo inajumuisha wachezaji 30 wa ndani na makipa wanne.
  Maandalizi hayo ya Serengeti Boys yatakwenda sambamba na kucheza mechi za kirafiki kabla ya kuhairisha kambi hiyo itakayokuwa ikifanyika mara kwa mara na mpango uliopo ni kila mwezi timu hiyo kuingia kambini.
  Serengeti Boys ipo chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen anayesaidiwa na Oscar Milambo na inajiandaa na michuano ya CECAFA Challenge U-17. 
  Wakati huo huo: Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  Wallace Karia amempongeza mwanamichezo, Dk Damas Ndumbaro kwa kushinda kiti cha Ubunge Jimbo la Songea Mjini.
  Rais Karia amesema ushindi wa Dk. Ndumbaro unaongeza wanamichezo zaidi katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wanaweza kuwa chachu ya maendeleo ya michezo ikiwemo mpira wa miguu.
  Amesema uzoefu wa Dk. Ndumbaro katika mpira wa miguu utasaidia katika nyanja hiyo na itasaidia kupaza sauti kupitia bunge katika harakati za kushirikiana kuusogeza mbele mchezo wa soka.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TISA WACHUJWA SERENGETI BOYS, KAMBINI KUVUNJWA JANUARI 28 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top