• HABARI MPYA

  Monday, January 15, 2018

  REFA ALIYEMPIGA TEKE MCHEZAJI UFARANSA ASIMAMISHWA

  REFA Tony Chapron amesimamishwa kuchezesha mechi nchini Ufaransa hadi suala lake litakapotolewa maamuzi na Kamati ya Nidhamu.
  Chapron jana alimpiga teke beki wa Nantes, Diego Carlos kabla ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano na kumtoa kwa nyekundu dakika ya 90 na ushei timu yake ikifungwa 1-0 na  Paris Saint-Germain katika mechi ya Ligue 1 Uwanja wa Beaujoire - Louis Fonteneau mjini Nantes.
  Sasa Tony Chapron hatakuwepo kazini Jumatano wakati wa mechi ya timu zinazopigana kuepuka daraja, Angers na Troyes.
  Shirikisho la Soka Ufaransa limethibitisha: "Bwana Tony Chapron, uteuzi wake wa kuchezesha mechi kati ya Angers dhidi ya Troyes umesitishwa kwenye mechi hiyo ya 21 jumatano ya Januari 17 hadi mwongozo utakapotolewa,”.
  Refa Tony Chapron akimuonyesha kadi nyekundu, beki wa Nantes, Diego Carlos jana

  "Chapron atakutana na kamati ya Nidhamu ya Bodi ya Ligi (LFP). Baada ya kupitia picha, Kamati imegundua Chapron hakuangushwa kwa makusudi,” amesema.
  Carlos anaweza kuruhusiwa kucheza mechi dhidi ya Toulouse Jumatano kwa mujibu wa taarifa.
  Carlos alikuwa tayari ana kadi ya njano wakati Paris Saint-Germain wanapeleka shambulizi la kujibu na mchezaji huyo Mbrazil mwenye umri wa miaka 24 akagongana na refa huyo wakati anakimbia kurudi kuihami timu yake isifungwe.
  Refa alikuwa anakimbia na mchezo na bahati mbaya akapamiana na Mbrazil huyo na kuanguka chini, lakini ajabu akainuka na kumrudishia kwa teke kabla ya kumuonyesha kadi mfululizo.
  Beki wa Nantes alionyesha uungwana kwa kumsaidia refa Chapron baada ya kuanguka, ingawa hiyo haikumsaidia kumuepusha na kadi na akawapa mpira wa adhabu PSG wapige. 
  PSG iliibuka na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo huo, bao pekee la winga Muargentina, Angel Di Maria dakika ya 12.
  Rais wa Nantes, Waldemar Kita ametaka refa Chapron afungiwe miezi sita.
  "Nimepokea SMS 20 duniani kote zikiniambia huyu refa ni wa ovyo,"alisema Kita akizungumza na L'Equipe.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA ALIYEMPIGA TEKE MCHEZAJI UFARANSA ASIMAMISHWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top