• HABARI MPYA

    Monday, January 15, 2018

    RYAN GIGGS NDIYE KOCHA MPYA MKUU WA WALES

    Ryan Giggs ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


    WASIFU WA GIGGS

    1990-2014: Manchester United
    1991-2007: Wales 
    2013-2014: Manchester United (Kocha Msaidizi)
    2014: Manchester United (Kocha wa Muda) 
    2018- hadi sasa: Wales (Kocha Mkuu) 
    MWANASOKA wa zamani wa kimataifa wa Wales, Ryan Giggs ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo.
    Gwiji huyo wa Manchester United amejitosa kwenye soka na uchambuzi tangu astaafu soka, lakini hakuwa kupata ajira rasmi. 
    Bodi ya nchi hiyo imemtihibitisha Giggs kuwa kocha mpya wa timu hiyo kupitia kwenye Twitter.
    Giggs alikuwa mmoja wa makocha wanne waliokuwa wanawania nafasi hiyo ambao walifanyiwa usaili Alhamisi- kocha wa sasa wa Sunderland, Chris Coleman, na mchezaji mwenzake wa zamani wa Wales, Craig Bellamy, Mark Bowen — ambyae ameondoka Stoke — na Msaidizi, Osain Roberts.
    Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 sasa atakuwa na jukumu la kuisaidia timu hiyo kufuzu Euro 2020, baada ya kushindwa kufuzu kwenye fainali za Kombe la Dunia Urusi 2018.
    Giggs aliichezea timu yake ya taifa mechi 64 na ninfuraha iliyoje kwake mwishowe anapata nafasi pia kuwa kocha. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RYAN GIGGS NDIYE KOCHA MPYA MKUU WA WALES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top