• HABARI MPYA

  Sunday, January 14, 2018

  MOROCCO YAANZA NA MOTO WA HATARI CHAN 2018

  WENYEJI Morocco na wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda taji wameanza vizuri Fainali za Michuano ya Ubingwa wa Matafa (CHAN) kwa kuitandika Mauritania 4-0 jana katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca.
  Katika mchezo huo wa ufunguzi, mshambuliaji  Ayoub El Kaabi akifunga mabao mawili dakika za 66 na 80 na mengine yakifungwa na Ismail El Haddad dakika ya 72 na Achraf Bencharki dakika ya 90 na ushei.
  Morocco iliwaanzisha wachezaji watatu wa kikosi cha Wydad Casablanca kilichoshinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka jana, lakini iliwaingiza washambuliaji wake nyota Achraf Bencharki na Walid el Karti dakika za mwishoni.

  Mshambuliaji Ayoub El Kaabi amefunga mabao mawili Morocco ikishinda 4-0 katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Mauritania 

  Mchezo mwingine wa Kundi A unafuatia leo kwa Guinea kumenyana na Uwanja wa Mohamed V pia. Mechi nyingine za leo ni za Kundi B kati ya Ivory Coast na Namibia Saa 1:30 usiku na Zambia na Uganda Saa 3:30 usiku zote Uwanja wa Marrakech.
  Ushindi wa Morocco jana ulikuwa ni sawa na kumuenzi nyota wake wa zamani, Hamid Hazzaz aliyefariki dunia kwa shinikizo la damu akiwa ana umri wa miaka 72 saa chache kabla ya michuano hiyo kuanza.
  Akifahamika kwa jina la utani kama "The Spider", Hazzaz alikuwemo kwenye kikosi cha Morocco kilichoshiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka 1970 na kikosi kilichoshinda Kombe la Mataifa ya Afrika miaka sita baadaye.
  Sherehe nzuri za ufunguzi ziliitangulia mechi ya kwanza na mtoto wa mfalme mwenye umri wa miaka 14, Prince Moulay el Hassan alifungua mashindano hayo. 
  Mfalme huyo mdogo pia alipeana mikono na kila mchezaji na marefa na akapiga picha na vikosi vya timu za Morocco and Mauritania.
  Washindi wa awali wa michuano hiyo inayofanyika kila baada ya miaka miwili ikishirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mara mbili, Tunisia na Libya. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOROCCO YAANZA NA MOTO WA HATARI CHAN 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top