• HABARI MPYA

  Sunday, January 14, 2018

  OLUNGA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO GIRONA KWA HAT TRICK

  MSHAMBULIAJI Mkenya, Michael Olunga jana amefunga mabao matatu na kuseti moja timu yake, Girona ikiitandika 6-0 Las Palmas katika mchezo wa La Liga Uwanja wa Manispaa ya Montilivi mjini Girona.
  Olunga, anayecheza kwa mkopo kutoka Guizhou Zhicheng ya China alifunga hat-trick yake katika dakika za 57, 70 na 79 na akatoa pia pasi ya bao la nne lililofungwa na Portu dakika ya 74.
  Mabao mengine ya Girona yalifungwa na Cristhian Ricardo Stuani Curbelo kwa penalti dakika ya 25 na Borja Garcia dakika ya 64.
  Mkenya Michael Olunga (katikati) akipongezwa na wenzake jana baada ya kufunga mabao matatu Girona ikiitandika 6-0 Las Palmas katika mchezo wa La Liga  

  Olunga amefunga kwa mara ya kwanza jana Girona katika mchezo wake wa tano na anaweza rekodi ya kuwa mchezaji wa klabu hiyo kufunga hat trick katika michuano mikubwa nchini Hispania. 
  Mechi nyingine za La Liga jana, bao pekee la Pablo Fornals dakika ya 87 lilitosha kuwapa Villarreal ushindi wa 1-0 dhidi ya Real Madrid Uwanja wa Bernabeu.
  Na bao pekee la mshambuliaji Mfaransa, Kevin Gameiro dakika ya 27 likaipa ushindi wa 1-0 Atletico Madrid dhidi ya wenyeji, Eibar Uwanja wa Manispaa ya Ipurua katika mchezo mwingine wa La Liga na 
  Deportivo La Coruna ikakubali kipigp cha 2-1 nyumbani kutoka kwa  Valencia.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OLUNGA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO GIRONA KWA HAT TRICK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top