• HABARI MPYA

  Tuesday, January 23, 2018

  DE BRUYNE ASAINI MKATABA MPYA MNONO NA MKEWE MAN CITY

  KLABU ya Manchester City imemsainisha mkataba mpya wa miaka mitano na nusu mchezaji wake nyota, Kevin De Bruyne.
  De Bruyne alikubali kusaini wiki iliyopita kwa mshahara wa Pauni 280,000 kwa wiki, ambao utamfanya awe anapokea na posho ya Pauni 70,000.
  Na hii inazima kabisa uwezekano wa mchezaji huyo kwenda Real Madrid na Barcelona zilizokuwa zinamhitaji pia kutokana na City kumtia pingu za miguu haraka hadi mwaka 2023.
  Na habari njema zaidi kwa kocha Mspaniola, Pep Guardiola ni kwamba kiungo Mbrazil, Fred mwenye umri wa miaka 24 anakaribia kujiunga na City kutoka Shakhtar Donetsk.


  Nyota wa Manchester City, Kevin De Bruyne akisaini mkataba mpya akiwa na mkewe, Michele PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  De Bruyne ametulia Jijini Manchester na mkewe, Michele na mwanawe wa kiume mdogo, Mason na anataka kumfanyia kazi nzuri Guardiola katika miaka hiyo karibu mitano.
  De Bruyne amefunga mabao 31 katika mechi 122 na kutoa pasi za mabao 50 tangu ajiunge na City kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 55 kutoka Wolfsburg Agosti mwaka 2015.
  De Bruyne anakuwa mchezaji wa tatu wa City kusaini mkataba mpya tangu wiki iliyopita baada ya Nicolas Otamendi na Fernandinho. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DE BRUYNE ASAINI MKATABA MPYA MNONO NA MKEWE MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top