• HABARI MPYA

  Monday, January 01, 2018

  ASHLEY YOUNG AFUNGIWA MECHI TATU MANCHESTER UNITED

  WINGA wa Manchester United, Ashley Young amefungiwa mechi tatu na Chama cha Soka England (FA).
  Katika taarifa yake ya jana Saa 3:00 usiku, FA imeiambia Manchester United kwamba, Young hatacheza mechi tatu kwa kufanya vurugu kwenye mechi dhidi ya Southampton Jumamosi.
  "Amekubali kosa la kufanya vurugu wakati mpira umesimama kwenye mchezo dhidi ya Southampton, lakini akasema adhabu ilikuwa kubwa. Hiyo ilikataliwa na Tume ya Kanuni," imesema taarifa ya FA.
  Ashley Young (kulia) amefungiwa mechi tatu na Chama cha Soka England 

  Young sasa atakosa safari ta mwaka mpya kwenda Everton, mechi ya Kombe la Emirates nyumbani kwa Derby County Ijumaa na mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Stoke City Januari 15.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ASHLEY YOUNG AFUNGIWA MECHI TATU MANCHESTER UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top