• HABARI MPYA

  Tuesday, December 19, 2017

  NJOMBE MJI YASAJILI WATANO WAPYA, WAWILI KUTOKA RWANDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Njombe Mji FC imesajini wachezaji wawili kutoka Rwanda kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Kocha wa Njombe Mji FC, Mlage Kabange ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba wachezajhi hao ni Herelimana Lewi kutoka Mukura Victory na Etienne Ngladjo kutoka Sunrise FC, zote za Rwanda.
  Pamoja na wawili hao kutoka Ligi Kuu ya Azam Rwanda, Kabange amesema pia wamewasajili wachezaji wengine watatu kwa mkopo kutoka timu tofauti.
  Nickson Kibabage anakwenda Njombe Mji FC kwa mkopo kutoka Mtibwa Sugar 

  Kabange winga wa zamani wa Simba ya Dar es Salaam amewataja wachezaji hao kuwa ni  Mohammed Titi kutoka Singida United, Nickson Kibabage na Muhsin Malima wote kutoka Mtibwa Sugar.
  Baada ya mapumziko ya wiki tatu kupisha michuano ya CECAFA Challenge iliyofikia tamati Jumapili nchini Kenya, Njombe Mji itateremka tena dimbani Desemba 31 kumenyana na Singida United kuanzia Saa 8:00 mchana Uwanja wa Saba Saba, Njombe.
  Kwa sasa, Njombe Mji wanashika nafasi ya 15 katika Ligi Kuu ya timu 16, ikiwa na pointi nane baada ya kucheza mechi 11.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NJOMBE MJI YASAJILI WATANO WAPYA, WAWILI KUTOKA RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top