• HABARI MPYA

  Sunday, December 17, 2017

  LIPULI YASAJILI WANANE WAPYA,YAWAACHA SITA AKIWEMO MACHAKU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Lipuli ya Iringa imeimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wanane wapya kwa ajili ya hatua ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Taarifa ya Lipuli FC imewataja wachezaji hao wapya ni pamoja na kiungo Jamal Mnyate aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Simba SC na Mghana, Alex Ntiri kutoka Mbao FC ya Mwanza.
  Wengine ni Adam Salamba kutoka Stand United, Miraji Mwilenga kutoka Mufindi United, Zawadi Mauya kutoka Mufindi United, Steven Mganga kutoka Pamba FC, Nelson Campbell na Feisal Salum Abdallah aliye na kikosi cha Zanzibar kwenye michuano ya CECAFA Challenge ambao wote ni wachezaji huru.
  Jamal Mnyate (kushoto) amekwenda Lipuli kwa mkopo kutoka Simba SC

  Pamoja na kufanikiwa kuwapata wanane hao wapya, Lipuli FC pia imewasajili Waziri Ramadhani, Mussa Ngunda, Machaku Salum, Melvin Alistoto, Ahmeid Manzi na Dotto Kayombo.
  Bado Lipuli iko kwenye mvutano na klabu ya Simba juu ya beki Mghana, Asante Kwasi. Kwasi inaaminika amesaini Simba akiwa bado ana mkataba na Lipuli.
  Kikosi cha Lipuli kinaendelea na mazoezi chini ya makocha wake, Amri Said ‘Stam’ na Suleiman Abdallah Matola kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIPULI YASAJILI WANANE WAPYA,YAWAACHA SITA AKIWEMO MACHAKU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top