• HABARI MPYA

    Friday, December 15, 2017

    HISPANIA HATARINI KUENGULIWA KOMBE LA DUNIA MWAKANI URUSI

    USHIRIKI wa Hispania kwenye Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi uko shakani kufuatia Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kuonya serikali ya nchi hiyo kuingilia shughuli za shirikisho la soka.
    FIFA imeliambia shirikisho la soka Hispania (RFEF) kwamba kuendelea kuihusisha serikali kwenye uchaguzi ujao wa Urais wa RFEF kutawaponza wafungiwe na wakose fainali zijazo za Kombe la Dunia. 
    Soka ya Hispania imekuwa ikiongozwa na Rais wa Muda, Juan Luis Larrea tangu Julai kufuatia aliyekuwa Rais, Angel Maria Villar kulazimishwa kujiuzulu kwa tuhuma za rushwa.
    Baada ya mapendekezo ya uchaguzi mpya kutolewa, serikali ya Hispania kupitia Baraza la Michezo la Taifa, limeiambia RFEF kumchagua Villar awe rais wa kudumu.
    Hispania iko hatarini kuenguliwa kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi

    FIFA imezuia namna yoyote ya Serikali kuingilia shughuli za soka na inaweza kumsimamisha mwanachama wake yoyote wa nchi yoyote kama uendeshwaji wake utaingiliwa na serikali.
    Villar alijiuzulu baada ya kukamatwa kwa tuhuma za rushwa Julai mwaka huu pamoja na mwanawe na Maofisa wengine watatu wa RFEF. 
    Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Hispania pia alijiuzulu wadhifa wake wa Umakamu Rais wa UEFA na Makamu wa Rais wa FIFA, ambako alikuwa chini ya Rais Mtaliano, Gianni Infantino.
    Rais wa zamani wa FIFA, Sepp Blatter alitaka kuifungia Hispania kutoshiriki Euro 2008, michuano ambayo waliibuka mabingwa kufuatia serikali ya Hispnia kutuhumiwa kuingilia shughuli za uchaguzi pia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HISPANIA HATARINI KUENGULIWA KOMBE LA DUNIA MWAKANI URUSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top