• HABARI MPYA

    Friday, December 15, 2017

    SINGIDA UNITED YAMSAJILI PAPAA KAMBALE, VIJANA 4 WA SERENGETI BOYS , DANNY LYANGA

    Na Slam Suleiman, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Singida imeimarisha safu yake ya ushambuliaji katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Daniel Lyanga kutoka Fanja ya Oman.
    Pamoja Lyanga, Singida United imemsajili mshambuliaji mwingine, Kambale Salita 'Papy Kambale' kuhakikisha wanakuwa na safu kali zaidi ya ushambuliaji katika hatua iliyosalia ya Ligi Kuu.
    Katika hatua za kuendeleza mpira nchini, klabu ya Singida United imewasaka na kuwapata vijana wanne walioshiriki Michuano mikubwa barabi Africa kwa vijana umri chini ya miaka 17 AFRICON 2017 waliokuwa na kikosi cha Serengeti Boys.
    Daniel Lyanga ameachana na Fanja ya Oman na kutua Singida United 

    Hatua hiyo ni moja ya mipango iliyowekwa na uongozi wa kusaidia vijana hasa wale ambao walishaonekana na hata kulipigania Taifa na baada ya michuano hiyo kumalizika wengi wao walitawanyika na kukosa timu za kusimama nao.
    Hivyo katika kulinda vipaji hivyo, Singida United imeamua kuchukua wachezaji wa nne kwa usajili wa miaka mitatu kila mmoja huku wakilipwa Signing fee,mshahara na allowance stahiki zao ili kuwajenga katika mfumo wa soka la ushindani.
    Vijana hao, mmoja ni kepteni wa Serengeti Boys, Issa Makamba, kiungo wa kati, Mwingine ni Assad Juma mshambuliaji ni mzaliwa wa Zanzibar, pia Ally Ng’azi beki na Mohamed Abdallah mshambuliaji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA UNITED YAMSAJILI PAPAA KAMBALE, VIJANA 4 WA SERENGETI BOYS , DANNY LYANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top