• HABARI MPYA

    Wednesday, October 04, 2017

    UGANDA YATANDIKWA 2-1 NA MADAGASCAR PALE PALE KAMPALA

    TIMU ya taifa ya Uganda, The Cranes leo imefungwa mabao 2-1 na Madagascar katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa StarTimes eneo la Lugogo mjini Kampala, Uganda.
    Kiungo wa timu ya KCCA, Muzamil Mutyaba alianza kuifungia The Cranes bao la kuongoza dakika ya 28, ambalo lilidumu hadi baada ya mapumziko.
    Rio Carlous Anoriananicinos akafunga mabao mawili kipindi cha pili, Madagascar ikiwastaajabisha Waganda kwa kutoka nyuma kwa 1-0 na kushinda 2-1 ugenini. Carlous alifunga mabao yake katika dakika za 49 na 88 kuipa Madagascar ushindi huo maarufu.
    Wachezaji wa Uganda, Emmanuel Okwi (7), Derrick Nsibambi (11) na Milton Karisa (23) wakipambana kwenye lango la Madagascar PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Benchi la Ufundi la Uganda Cranes likiongozwa na kocha wa zamani wa klabu ya Simba ya Tanzania, Moses Basena lilitumia vikosi viwili tofauti kila kipindi.
    Nahodha na kipa wa kwanza, Dennis Onyango ndiye mchezaji pekee ambaye hakutumika leo.
    Kikosi cha Uganda kitaendelea na mazoezi kesho Uwanja wa Taifa wa Mandela Saa 10:00 jioni kujiandaa na mchezi wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ghana Jumamosi mjini Kampala.
    Vikosi vya Uganda vilikuwa; kipindi cha kwanza: Ismail Watenga, Denis Iguma, Godfrey Walusimbi, Savio Kabugo, Isaac Isinde, Tonny Mawejje, Hassan Wasswa Mawanda, William Luwagga Kizito, Muzamiru Mutyaba, Edrisa Lubega na Joseph Ochaya
    Kipindi cha pili; Benjamin Ochan, Nico Wakiro Wadada, Isaac Muleme, Bernard Muwanga, Milton Karisa, Emma Okwi, Geoffrey Serunkuma, Ivan Ntege, Farouk Miya, Timothy Awanyi na Derrick Nsibambi.
    Madagascar: Ibrahim Dabo, Ranbelosn Toavina, Pascal Razakanantenaina, Thomas Fontaine, Nonenjana Lalaina/Patrick Herimanjaarivo dk62, Jean Raherinarimanana, Calsin  Dimitry, Randrinbololuna Zotsara, Rio Carlous Anoriananicinos, Ina Faneva Andriatsina na Ferdinard Ramananahera/Hery Randriaitara dk75.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UGANDA YATANDIKWA 2-1 NA MADAGASCAR PALE PALE KAMPALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top